• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Raga ya Impala Floodlit kurejea Oktoba baada ya miaka miwili

Raga ya Impala Floodlit kurejea Oktoba baada ya miaka miwili

NA GEOFFREY ANENE

MAKALA ya 38 ya raga ya Impala Floodlit yataandaliwa Oktoba 29, Novemba 5 na Novemba 12 katika klabu ya Impala mjini Nairobi.

Mashindano haya hutumiwa na klabu kupasha misuli moto kabla ya msimu mpya wa raga ya wachezaji 15 kila upande. Yanarejea baada ya miaka miwili. Hayufanyika 2020 kwa sababu ya mkurupuko wa virusi vya corona na ukosefu wa fedha mwaka 2021.

Mwenyekiti wa klabu ya raga ya Impala, Charles Ngovi alisema Ijumaa, “Tunafurahi sana Impala Floodlit inarejea baada ya miaka miwili.”

Makala ya 2022 yamevutia timu 22 zitakazoshindana katika vitengo vitatu – wanawake, vyuo vikuu na klabu. Vitengo vya vyuo vikuu na klabu vitakuwa na timu nane kila kimoja kutoka timu zinazoshiriki Ligi Kuu, Ligi ya Daraja ya Pili na Ligi Pana, huku kile cha kinadada kikikutanisha timu sita.

Mkurugenzi wa mashindano Daniel Ndaba amesema maandalizi ya mashindano hayo yamepamba moto, tayari kuletea mashabiki, wachezaji na washiriki burudani la kufana.

“Tutatangaza orodha ya washiriki wakati wa droo mnamo Oktoba 21,” alisema. Bei ya tiketi za mapema ni Sh300 kwa wikendi mbili za kwanza halafu Sh400 wikendi ya fainali. Zinaweza kununuliwa kwenye tovuti ya www.Kenyabuzz.com.

Matokeo ya Impala Floodlit 2019:

Fainali ya Shule za Upili – Ofafa Jericho 21 Muhuri Muchiri 0

Fainali ya Wanawake – Black Panther 5 Black Lions 40

Fainali ya Vyuo Vikuu – Mean Machine 16 Strathmore Leos 26

Klabu (Sahani) – Impala Saracens 17 Nondies 15

Klabu (Nambari tatu na nne) – Kenya Harlequin 5 Homeboyz 30

Klabu (Fainali) – KCB 23 Menengai Oilers 9

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Sera mpya ya kifedha ya Ruto itaokoa raia wengi

Ebola: Madereva na wageni Moi International Airport jijini...

T L