• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Rangers na Slavia nguvu sawa katika mkondo wa kwanza Europa League

Rangers na Slavia nguvu sawa katika mkondo wa kwanza Europa League

Na MASHIRIKA

RANGERS walitoka nyuma kwa bao moja na kuwalazimishia Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech sare ya 1-1 katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya Europa League mnamo Alhamisi.

Chini ya kocha Steven Gerrard ambaye ni kiungo na nahodha wa zamani wa Liverpool, Rangers waliwaendea Slavia siku nne baada ya kutia kapuni ubingwa wa Ligi Kuu ya Scotland. Slavia ndio waliowadengua Leicester City ya Uingereza kwenye hatua ya 32-bora ya Europa League msimu huu.

Rangers walijipata nyuma baada ya dakika sita pekee kutokana na goli lililopachikwa wavuni na Nicolae Stanciu.

Hata hivyo, Filip Helander alisawazishia Rangers katika dakika ya 36 na kuwaweka waajiri wake pazuri zaidi kusonga mbele kwa hatua ya robo-fainali kabla ya marudiano yatakayoandaliwa mnamo Machi 18 jijini Ibrox, Scotland.

Kipa Allan McGregor alifanya kazi ya ziada mwishoni mwa kipindi cha pili kwa kupangua makombora mazito kutoka kwa washambuliaji wa Slavia na kuhahakisha kwamba mechi hiyo inakamilika kwa sare ya 1-1.

Rangers wamejivunia msimu wa kuridhisha katika kampeni wanazozishiriki msimu huu ikizingatiwa kwamba bado hawajapotez mechi yoyote kwenye soka ya bara Ulaya katika muhula huu wa 2020-21.

Rangers sasa watapumzika kwa wiki nzima bila ya kusakata mchuano wowote kabla ya kushuka ugani kurudiana na Slavia katika uwanja wao wa nyumbani jijini Ibrox mnamo Alhamisi ya Machi 18, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Vipusa wa Man-City wakomoa Fiorentina 8-0 na kufuzu kwa...

TAHARIRI: Uamuzi wa kafyu uzingatie usalama