• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Selina wa vishale anatamba kote nchini

Selina wa vishale anatamba kote nchini

NA JOHN KIMWERE

KWA wengi, vishale ni mchezo wa starehe za pombe kilabuni.

Huchukuliwa kuwa wa wanaume kupitisha muda wakijipa dozi kadhaa.

Lakini kwa Selina Nyaboke Sakawa, vishale ni njia ya kujikimu kimaisha, sawa tu na fani nyingine kama riadha, soka na gofu.

Sakawa, 48, ni kati ya wanadada wachache wanaovumisha mchezo huo nchini kwa umahiri.

Mwanzo wa ngoma alipiga voliboli na klabu ya Posta mjini Kisii, kabla kugeukia vishale 1995.

Katika vishale alianza kuchezea klabu ya KASU huko huko Kisii.

“Nilihisi mchezo wa vishale ndio ungeimarisha kipawa changu, baada ya kutazama wachezaji maarufu wakishiriki,” aliambia Dimba.

Wakosoaji na wasioamini hawakumdhania angeibuka kuwa staa, lakini mama huyu wa watoto wanne amekolea nchini.

“Itakuwa furaha kubwa kwangu kupimana na vigogo wa nchi zilizo gwiji kama Canada na Amerika, ambako vishale inalipa vizuri kinyume na ilivyo barani Afrika,” anahoji.

Ustadi wake, anaeleza, umechangiwa pakubwa na hatua yake ya kushiriki mazoezi dhidi ya wachezaji wa kiume katika klabu ya Magereza. Sakawa ndiye mwanavishale namba wani kitengo cha wanawake.

Selina Sakawa anayeng’aa vishale. PICHA | JOHN KIMWERE

Anajivunia mataji mengi zaidi ya 10 ya kiwango cha Singles, katika mashindano ya humu nchini na pia michuano ya kanda ya frika Mashariki na Kati.

Mwaka huu 2021, Sakawa alijiunga na klabu ya Museum kama mkufunzi wa timu ya Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kwa mwaka mmoja.

Alikuwa amechezea timu hiyo tangu 2010 hadi 2021.Kando na KASU, CAK dada huyu amechezea klabu kibao ikiwamo Sony Sugar, Kenya Commercial Bank (KCB), Halmashauri ya viwanja vya ndege (KAA), na klabu ya chuo cha mafunzo ya maafisa wa utawala (APTC).

You can share this post!

STAA WA SPOTI: Spidi yake kali ilimtoa katika voliboli na...

UDA yakataa madai kuhusu ugavi wa mamlaka

T L