• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Talanta ya soka ilimpa fursa ya kusoma kupitia ufadhili na kumpa nafasi ya kujikuza

Talanta ya soka ilimpa fursa ya kusoma kupitia ufadhili na kumpa nafasi ya kujikuza

NA PATRICK KILAVUKA

MWANAKANDANDA Yassin Robert, 26, anasema soka ilimfaa sana maishani kwa sababu ndio ilimwezesha kusoma ikizingatiwa talanta yake ilimpa nafasi ya kuiwakilisha shule ya msingi hadi upili kwa matao.

Alianza kusakata boli kama winga kabla kudhibiti nafasi ya kiungo katika timu mbalimbali.

Mwanasoka huyu ni mzaliwa wa Gitie, Imenti ya Kati, Kaunti ya Meru.

Alipata masomo yake shule ya msingi ya Gitie kabla kujiunga na Shule ya Upili ya Wavulana ya Kanyakine.

 

Talanta ya soka ilimpa Yassin Robert fursa ya kusoma kupitia ufadhili na akapata nafasi ya kujikuza. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Ni akiwa shule ya sekondari ambapo alidhamini na Betika kujiunga na akademia ya soka ya Talanta Academy alikodumu kutoka mwaka 2019- 2021.

Ingawa hivyo, alikuwa kambi ya timu ya Gitie Young Stars alikocheza kama winga na wakati timu hiyo ilipokuwa inashiriki Ligi yaFKF, Kaunti Ndogo ya Imenti ya Kati.

Hatimaye, alichezea timu ya Mitungu FC ambayo ilikuwa inashiriki ngarambe ya Ligi ya Divisheni ya Pili.

Mwanadimba Robert anakumbuka malezi ya kisoka kutoka kwa makocha Mwalimu Franklin Mwenda akiwa shule ya upili, Yusufu Juma akiwa Mitungu na Jamal Sharch akiwa Isiolo ambao wamekumbatia talanta yake.

Mwaka huu 2022 amepata fursa ya kusajiliwa katika timu ya Real Stars chini ya kocha Ominde baada ya mkufunzi huyo kuona wazi uhitaji wa mchezaji ambaye angedhibiti safu ya kiungo kwani anasema aliuliza wachezaji wake kama wanaweza kuwa na mchezaji ambaye anaweza kuwasaidia kukasa nati za kiungo na ndugu ambaye analewa tajriba akamdokeza mkufunzi huyo kumhusu na akafanywa majaribio na kuonesha weledi wake na hatimaye kujumuishwa kiotani.

Mwanadimba Yassin Robert (wa kwanza kushoto pichani) katika kikosi cha klabu ya Real Stars ya Kangemi, ambayo inashiriki ligi ya Kaunti ndogo ya FKF, Nairobi West. PICHA | PATRICK KILAVUKA

“Ni wakati wa mazoezi kwa mara ya kwanza, aliuwiana vyema na wachezaji wangu na nilimtambua zaidi na nikakata kiu cha kumtafua kiungo mwengine. Sasa ninamwandaa vyema katika mfumo wa timu na ninatazamia atakuwa mpesi wa kukolea timu,” akafafanua kocha Ominde ambaye timu yake inashiriki Ligi ya Kaunti Ndogo, FKF, Nairobi West.

Angependa kuwashiriki mishenari Daniel Scarinantor kwa ufadhili pia akiwa shule ya msingi kwa sababu ya yeye aliihusudu talanta yake na kumtakia mwema katika kuikuza pasi na kuchelea kuona pili anasoma.

Yeye ni shabiki mkuu wa timu ya Liverpool anakocheza kiungo Thiago Alcântara ingawa kenya anavutiwa sana na upigaji soka wa mshambulizi Michael Olunga ambaye anatesa ughaibuni.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Uchaguzi: Raia waitikie wito wa kujitokeza kwa...

Raila chaguo la wengi – tafiti za hivi punde

T L