• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Timu ya taifa ya Ghana yapokeza Chris Hughton mikoba ya ukocha

Timu ya taifa ya Ghana yapokeza Chris Hughton mikoba ya ukocha

Na MASHIRIKA

KOCHA wa zamani wa Brighton, Chris Hughton, ameteuliwa kudhibiti mikoba ya timu ya taifa ya Ghana.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 64 amekuwa mshauri wa benchi ya kiufundi ya Ghana almaarufu Black Stars tangu Februari 2022.

Anajaza pengo la Otto Addo aliyejiuzulu mwishoni mwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar, ambapo Ghana walivuta mkia wa Kundi H baada ya kushinda mechi moja pekee kati ya tatu.

Hiki ni kibarua cha kwanza kwa Hughton katika ulingo wa ukufunzi tangu apigwe kalamu na kikosi cha Nottingham Forest mnamo Septemba 2021.

Aliwahi pia kunoa vikosi vya Newcastle, Birmingham na Norwich kabla ya kuhudumu kambini mwa Brighton kwa kipindi cha miaka mitano na kuongoza kikosi hicho kupanda ngazi kutoka Ligi ya Daraja ya Kwanza (Championship) hadi Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

George Boateng na Mas-Ud Didi Dramani wataendelea kuwa wakufunzi wasaidizi kambini mwa Ghana.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

Presnel Kimpembe aomba mashabiki msamaha baada ya kikosi...

Kujifungua Lamu ni hali ya kufa-kupona

T L