• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 11:13 AM
KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Tunisia wakosa kuingia 16-bora licha ya kuangusha miamba Ufaransa katika Kundi D

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Tunisia wakosa kuingia 16-bora licha ya kuangusha miamba Ufaransa katika Kundi D

Na MASHIRIKA

UFARANSA walishuhudia bao lao la kusawazisha dhidi ya Tunisia likifutiliwa mbali na teknolojia ya VAR mwishoni mwa kipindi cha pili katika pambano la Kundi E lililowakutanisha ugani Education City mnamo Jumatano.

Licha ya ushindi huo dhidi ya mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Tunisia waliotawazwa wafalme wa Kombe la Afrika (AFCON) 2004, walikosa kufuzu kwa hatua ya 16-bora baada y Australia kuzamisha Denmark 1-0 katika mchuano mwingine wa Kundi D.

Nahodha Wahbi Khazi aliweka Tunisia kifua mbele katika dakika ya 58 kabla ya goli la Antoine Grizemann wa Ufaransa kutohesabiwa.

“Ni matokeo ambayo yametupa hisia mseto. Tuna furaha ya kupepeta Ufaransa ambao ni wafalme wa dunia na tunasikitika kuondolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia katika hatua ya makundi,” akasema kocha wa Tunisia, Jalel Kadri.

“Ingekuwa tija na fahari zaidi kuingia raundi ya muondoano kwa mara ya kwanza katika historia. Lakini tumejifunza jambo. Tulikosa kufanya tulichostahili kufanya mwanzoni mwa kampeni za Kundi D,” akaongezea.

Ufaransa walishuka dimbani dhidi ya Tunisia tayari wakijivunia kuingia hatua ya 16-bora baada ya kutandika Australia 4-1 na kupepeta Denmark 2-1 katika mechi zao za ufunguzi wa Kundi D.

Kwa upande wao, Tunisia walianza kampeni zao za makundi kwa sare tasa dhidi ya Denmark kabla ya Australia kuwapokeza kichapo cha 1-0 katika pambano la pili.

Chini ya kocha Didier Deschamps, Ufaransa sasa watavaana na Poland katika hatua ya 16-bora mnamo Disemba 4 ugani Al Thumama huku Australia wakivaana na Argentina waliodhibiti kilele cha Kundi C lililojumuisha pia Saudi Arabia na Mexico.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Raila kupewa mamlaka iwapo Mswada utapita

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Argentina watinga hatua ya 16-bora

T L