• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:55 AM
UEFA: Huenda Aguero asicheze kwenye fainali ya Machester City dhidi ya Chelsea

UEFA: Huenda Aguero asicheze kwenye fainali ya Machester City dhidi ya Chelsea

Na MASHIRIKA

KOCHA Pep Guardiola amesema kwamba mshambuliaji Sergio Aguero hana uhakika wowote wa kutandaza mchuano wake wa mwisho wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) akivalia jezi za Manchester City msimu huu.

Aguero ambaye ni raia wa Argentina atabanduka rasmi ugani Etihad mwishoni mwa msimu huu baada ya kuchezea Man-City kwa kipindi cha miaka 10.

Kufikia sasa, sogora huyo wa zamani wa Atletico Madrid bado hayuko katika fomu nzuri ya kuwajibishwa dhidi ya Everton katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Mei 23 ugani Etihad.

Guardiola amedokeza uwezekano wa kutomtegemea Aguero kwenye fainali ya UEFA itakayowakutanisha na Chelsea mnamo Mei 29 jijini Porto, Ureno.

“Nitateua kikosi ambacho ninaamini kwamba kitatushindia taji la UEFA. Iwapo Aguero atakuwa katika hali nzuri ya kucheza, basi atapata nafasi. La sivyo, basi atasalia nje licha ya kwamba gozi hilo litampa fursa ya kutuchezea kwa mara ya mwisho muhula huu,” akasema Guardiola kwa kusisitiza kwamba jeraha la Aguero bado ni baya licha ya kwamba fowadi huyo amerejelea mazoezi mepesi.

Aguero hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na Man-City dhidi ya Brighton mnamo Mei 18 kwenye kipute cha EPL kitakachochezewa ugani American Express.

Nyota huyo anayeuguza jeraha la mguu, pia alikosa mechi ya Mei 14 dhidi ya Newcastle United na aliondolewa uwanjani baada ya dakika 70 kwenye gozi lililowashuhudia waajiri wake wakipigwa 2-1 na Chelsea ligini mnamo Mei 8 uwanjani Etihad.

Baada ya kampeni zake za msimu huu kutatizwa na majeraha mabaya, Aguero amefunga mabao manne pekee kutokana na michuano 18 na alipoteza penalti katika mchuano uliopita dhidi ya Chelsea.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Idadi ya chini ya wapigakura yashuhudiwa eneobunge la Juja

Jeraha la goti kumnyima kigogo Zlatan Ibrahimovic uhondo wa...