• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Wanaraga wa kike wa Kenya wapoteza vibaya dhidi ya Afrika Kusini

Wanaraga wa kike wa Kenya wapoteza vibaya dhidi ya Afrika Kusini

Na GEOFFREY ANENE

KENYA Lionesses wamepokea kichapo kikali cha pointi 77-12 Jumamosi mikononi mwa wenyeji Afrika Kusini katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa wa mashindano ya dunia ya daraja la tatu (WXV3) yatakayofanyika mwezi ujao wa Oktoba.

Vipusa wa kocha Dennis Mwanja waliporomoka katika kipindi cha pili baada ya
kuenda mapumzikoni wakiwa nyuma 24-12.

Ni kipigo cha tano mfululizo cha Lionesses dhidi ya Afrika Kusini katika raga ya wachezaji 15 kila upande baada ya kulimwa 39-0 (Agosti 17, 2019), 66-0 (Agosti 12, 2021), 29-22 (Agosti 16, 2021) na 48-0 (Mei 24, 2023).

Wakenya wanajiandaa kwa mashindano ya dunia ya daraja la tatu ambapo watalimana na Uhispania (Oktoba 14), Kazakhstan (Oktoba 20) na Colombia (28) ugani The Sevens jijini Dubai nchini Milki za Kiarabu.

Afrika Kusini pia wanajiandaa kwa mashindano ya dunia ya daraja la pili
dhidi ya Italia, Japan, Samoa, Scotland na Amerika mnamo Oktoba 13-28 mjini Cape Town.

  • Tags

You can share this post!

Liverpool watoka nyuma na kuendeleza masaibu ya Wolves...

Serikali yaombwa kuwaondolea raia mzigo wa gharama ya juu...

T L