• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
Zetech Sparks yalenga kusuka kikosi ipate kani kali za sumaku

Zetech Sparks yalenga kusuka kikosi ipate kani kali za sumaku

NA TOTO AREGE

KOCHA wa klabu ya Zetech Sparks Bernard Kitolo, ametoa wito kwa wachezaji wa soka wanaotaka kujiunga na timu hiyo kujitokeza kufanyiwa mchujo Jumanne ijayo ugani Ruiru katika Kaunti ya Kiambu.

Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), inapanga kuachilia wachezaji saba na kusajili majembe mengine saba.

Kitolo ambaye aliongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya sita na alama 32 kwenye msimamo wa ligi msimu wa 2022/23, anapanga kusajili kipa mmoja, beki wa katikati wawili, wing’a na mshambulizi mmoja pamoja na viungo.

Akizungumza na Taifa Spoti mnamo Alhamisi kwa njia ya simu, alisisitiza kuwa anajaribu kurekebisha makosa yao ya msimu jana.

“Msimu jana nilipoteza wachezaji wa kikosi cha kwanza dakika za mwisho. Ilinichukua muda mrefu kupanga kikosi kingine ambacho hakikufanya vizuri kwenye ligi,” alisema Kitolo.

“Nilipopata wachezaji wageni kwenye mechi za mkondo wa pili, kulikuwa na ushindani mkali ambao ulifanya wachezaji wangu wajitume zaidi kwenye ligi na walituondoa kwenye shoka la kushuka daraja,” aliongezea Kitolo.

Aidha anasema msimu jana, kipa tegemeo Monicah Karabu hakuwajibika kikosini kutokana na sababu za ndani.

  • Tags

You can share this post!

Jubilee: Kanini nje, Kioni ndani tena

Serikali yaonya Raila kuhusu maandamano

T L