• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 6:55 AM
Esther Gathogo asema alijihisi kama mfungwa ndani ya UDA

Esther Gathogo asema alijihisi kama mfungwa ndani ya UDA

NA SAMMY WAWERU

ALIYEKUWA mbunge wa Ruiru, Esther Nyambura Gathogo amefichua sababu zilizomshawishi kuhama kutoka United Democratic Alliance (UDA), chama kinachoongozwa na Naibu Rais Dky William Ruto, miezi miwili baada ya kujiunga nacho mapema mwaka huu, 2022.

Mwezi Januari mwanasiasa huyo alijiunga na UDA, na kufikia mwishoni mwa Machi akatangaza kugura na kuhamia Jubilee.

Akitetea maamuzi hayo, Bi Gathogo amesema chama hicho kina ‘wenyewe’.

“Nilikaa nikaambiwa kuna wale waanzilishi na wanaodandia. Nilipofanya mahesabu, nikaona mimi ni wa kudandia,” akafichua.

Alisema hayo kwenye mkutano na wamiliki na wahudumu wa tuktuk eneo la Githurai, akiomba wafanyabiashara hao Agosti 9 kumchagua awe mbunge wa Ruiru.

Gathogo aliongoza eneobunge hilo 2013 hadi 2017, na katika uchaguzi mkuu wa 2017 alipoteza wadhifa wake kwa mbunge wa sasa, Bw Simon King’ara.

Aliwania kama mgombea wa kujitegemea, naye King’ara kupitia tikiti ya Jubilee.

Bi Gathogo alisema wengi wamekuwa wakimtaka atoe sababu za kukita kambi UDA miezi michache, kisha akabadilisha msimamo ghafla.

“Wengi waliona nimevaa rangi fulani, wakati ukafika nikabadilika. Wakauliza, ni nini mama? Ninawajibu: Wewe kama ndio mimi, unong’onenezewe kama 2017 uambiwe pale mbele kuna shimo, ambapo nilipuuza ushauri nikasema mimi ndio huzika mashimo, kumbe nitazikwa na hilo shimo. Utaendelea kukaa mahali unaonywa kuna hatari?” akauliza.

UDA ni miongoni mwa vyama tanzu vinavyounda mrengo wa Kenya Kwanza, Dkt Ruto akiwa ndiye wa kupeperusha bendera ya urais.

  • Tags

You can share this post!

Ngirici amteua mhasibu kuwa mgombea mwenza

Salah na De Bruyne kati ya masogora wanane wanaowania taji...

T L