• Nairobi
  • Last Updated May 29th, 2023 9:37 PM
Gachagua: Raila apige tu picha na Rais, hakuna kuingia serikalini

Gachagua: Raila apige tu picha na Rais, hakuna kuingia serikalini

NA NDUBI MOTURI

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amesisitiza hakuna nafasi yoyote serikalini kwa kiongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga.

Amesema hayo Alhamisi akihutubia washirikishi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachoongozwa na Rais William Ruto, ambao wamekongamana katika hoteli ya Weston jijini Nairobi.

Amesema muunganpo tawala wa Kenya Kwanza unaruhusu Bw Odinga kupiga picha na Rais Ruto.

“Bw Odinga ajitokeze kupiga picha na Dkt Ruto wakati wowote, siku yoyote lakini afahamu kwamba hataruhusiwa kuingia serikalini kupitia ‘handisheki’,” amesema Bw Gachagua.

Mnamo Jumanne kiongozi wa Azimio alihutubia wanahabari katika Wakfu wa Jaramogi Oginga Odinga jijini Nairobi ambapo alitaka viongozi wa Kenya Kwanza wafahamu “sina haja na handisheki na Ruto.”

  • Tags

You can share this post!

DPP Haji apinga kufunguliwa kwa akaunti 30 za Pasta Odero,...

Idadi ya waliothibitishwa kufariki Shakahola yagonga 235

T L