• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 10:50 AM
Jubilee njiapanda maelewano kati ya wawaniaji yakifeli

Jubilee njiapanda maelewano kati ya wawaniaji yakifeli

NA ALEX NJERU

CHAMA cha Jubilee kinakabiliwa na hatari ya kupoteza wagombeaji katika kaunti ya Tharaka Nithi, baada ya mazungumzo ya kuteua wagombeaji kupitia maelewano kufeli.

Chama hicho, ambacho hakiko tayari kuwahusisha wapigakura katika uteuzi wa wawaniaji bora, kilishikilia kuwa kitatumia maelewano kuteua wale watakaopambana na wawaniaji kutoka vyama vingine.

Lakini wawaniaji wamepinga mfumo huo uliopendekezwa na uongozi wa Jubilee, huku wakiendelea na mchakato wa kujipigia debe kudhihirisha ushawishi wao.

Kulingana na ratiba, Jubilee itaanza kura ya mchujo kote nchini huku ikilenga kutimiza tarehe ya makataa ya Aprili 22.

Mwaniaji wa Useneta, Dkt Kunga Ngece, anayetoka eneo bunge la Chuka Igambang’ombe, anang’ang’ania tikiti ya Jubilee na Bw Paul Mugambi kutoka eneo bunge la Tharaka.

Dkt Ngece alisema sharti chama hicho kiteue mwaniaji mwenye ushawishi mkubwa ndiposa kiweze kumshinda atakayeteuliwa na chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Chama hicho kinachoongozwa na Naibu Rais William Ruto ni maarufu zaidi katika kaunti hiyo.

Mbunge wa zamani Petkay Miriti na Bi Mercy Kirit, ambao wanasaka tikiti ya UDA kuwania kiti hicho cha useneta, pia walitaka chama hicho kuendesha mchujo huru na haki.

Chama cha UDA kitaendesha kura ya mchujo kote nchini mnamo Aprili 14.

“Hata kama UDA itatumia mbinu ya kura ya maoni kuamua mgombeaji wake, sharti shughuli hiyo iendeshwe kwa njia huru na haki,” Bi Mercy akasema.

Naye Dkt Ngece aliitaka Jubilee kutumia mbinu ya uteuzi ambayo itawaridhisha wawaniaji wote.

Katika eneo bunge la Maara, chama cha Jubilee kinakabiliwa na kibarua kigumu kuamua mwaniaji bora kati ya Mbw Lawrence Kaburu na Hassan Kithinji.

  • Tags

You can share this post!

Migawanyiko DP Muturi akijiunga na Ruto

Brentford yazamisha chombo cha West Ham United ligini

T L