• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 6:50 AM
Junet hakula hela za maajenti – Azimio

Junet hakula hela za maajenti – Azimio

NA WANDERI KAMAU

KIONGOZI wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga, amewatetea vikali baadhi ya washirika wake kwa tuhuma kwamba walipora fedha zilizopangiwa kuwalipa maajenti wa muungano huo kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Baadhi ya washirika wake ambao wamekuwa wakielekezwa lawama hizo ni mbunge Junet Mohamed (Suna Mashariki), aliyekuwa gavana wa Mombasa Hassan Joho na Afisa Mkuu Mtendaji wa Sekretariati ya Azimio, Bi Elizabeth Meyo.

Bw Mohamed ndiye Katibu Mkuu wa Sekretariati hiyo.

Tangu matokeo ya uchaguzi huo, washirika wakuu wa Bw Odinga wamekuwa wakielekezeana lawama kuhusu yule aliyechangia kushindwa kwa muungano huo.

Lakini Jumapili, Bw Odinga aliwatetea vikali washirika hao, akiwataka wale wanaoeneza uvumi huo kukoma mara moja.

Kupitia msemaji wa Sekretariati ya kampeni zake, Prof Makau Mutua, Bw Odinga alisema washirika hao walitekeleza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.

“Msimamo wetu ni kuwa kundi hilo liliendesha utendakazi wake kwa njia nzuri sana katika mazingira magumu sana. Tungetaka kutaja kuwa si suala la maajenti lililochangia matokeo ya uchaguzi huo. Ulinzi wa kura ni jukumu la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwani ndiyo taasisi inayopaswa kuendesha uchaguzi kwa njia huru na yenye uwazi,” akasema Prof Mutua.

  • Tags

You can share this post!

Waomba usaidizi kurejesha mwili wa binti yao

TALANTA: Wanasarakasi ibuka

T L