• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 2:03 PM
‘Jungle’ Wainaina ateuliwa kinara wa IPLF kuangazia maslahi ya wagombea wa kujitegemea

‘Jungle’ Wainaina ateuliwa kinara wa IPLF kuangazia maslahi ya wagombea wa kujitegemea

NA LAWRENCE ONGARO

VIONGOZI wapatao 300 wanaotafuta nafasi za kisiasa wamejipanga katika kikundi cha wawaniaji wa kujitegemea ili kulinda maslahi yao.

Viongozi hao wamebuni kikundi cha Independent Political Leaders Forum (IPLF) kitakachowapa mwelekeo wao wa kisiasa.

Wanachama wa kikundi hicho walikongamana Thika mwishoni mwa wiki jana ili kujadiliana kuhusu hatima yao ya baadaye baada ya mchujo uliyoendelea hivi majuzi wa vyama vya kisiasa.

Wakati wa hafla hiyo mbunge wa Thika, Bw Patrick Jungle Wainaina, aliteuliwa kuwa kinara wa kikundi hicho cha IPLF.

Walisema hicho ni kikundi kitakacholeta mabadiliko katika uongozi wa nchi kwani wanalenga kuzoa viti asilimia 30 katika bunge, kwa viti vya useneti na ubunge.

“Sisi kama viongozi wa kujitegemea tunataka kuleta mabadiliko makubwa mbungeni ambapo nguvu yetu pia itakuwa na umuhimu mbungeni,” alifafanua Bw Wa ‘Jungle’ ambaye ni mbunge wa Thika.

Walisema kuwa viongozi wanaochaguliwa kupitia tikiti ya kujitegemea huwa wako huru kutoa maamuzi yao bila kushinikizwa na kiongozi yeyote wa chama cha kisiasa.

Walisema wataendelea kuzungumza kwa sauti moja ili waweze kutumikia wananchi kwa njia ifaayo.

Walieleza kuwa lengo lao kuu ni kutumikia mwananchi kwa njia ifaayo na kuhakikisha ananufaika mashinani.

Wakati wa hafla hiyo walimuidhinisha Bw Patrick Wa ‘Jungle’ Wainaina kuwania wadhifa wa gavana wa Kiambu kwa tiketi ya kujitegemea, naye Loise Kim, atawakilisha wanawake Kiambu endapo atachaguliwa, halafu wakili Wanjiku Mathai kuwania kiti cha ubunge Kiambu.

Wote pia walikubaliana jinsi ya kuwateua wawakilishi wa wadi (MCAs), na viti 11 vya ubunge Kiambu na kile cha Seneta.

Kikundi hicho cha IPLF, pia kilikubaliana kwa pamoja ya kwamba watakuwa wakifanya mikutano ya kila mara ili kujadiliana maswala yanayowakumba kama viongozi.

Walieleza pia kuwa watazuru maeneo mengine nchini ili kufanya mikutano na viongozi wengine ambao pia wangetaka kujiunga nao.

Wengi wa viongozi hao wakipewa nafasi ya kujieleza huku kila mmoja akitoka katika mkutano huo akiwa ameridhika.

  • Tags

You can share this post!

Wahudumu wa teksi mjini Thika watoa malalamishi ya kupokea...

Mashauriano yafanywa kuinua uchumi baharini

T L