• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 12:59 PM
Kenya Kwanza wamepoteza dira, asema Raila

Kenya Kwanza wamepoteza dira, asema Raila

NA NDUBI MOTURI

KIONGOZI wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga amesema Jumamosi kwamba serikali ya Kenya Kwanza imepoteza dira kwa kufanya mambo kinyume kabisa na ahadi za wakati wa kampeni.

Bw Odinga alikuwa akihutubu kwenye kikao cha Baraza la Azimio kutathmini utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza baada ya kuwa uongozini kwa mwaka mmoja.

“Tuliwaona hapa na pale wakitoa ahadi lakini sasa mambo yamebadilika ghafla na kwa hakika Wakenya hawajaridhishwa iwe ni katika kilimo, elimu, masuala ya kawi na fursa za vijana,” amesema Bw Odinga.

Kigogo huyo wa upinzani ameelezea hofu yake kuwa gharama ya maisha itazidi kupanda.

Aidha amesema kwamba gharama za matumizi kuenda kuzindua miradi ya maendeleo na viongozi serikalini zinapiku kiwango kilichotumika kutekeleza miradi hiyo.

“Vijana kote nchini na haswa eneo la Mlima Kenya wametumbukia kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa kukosa kazi ya maana ya kufanya… Unawezaje ukamwadhibu kijana ambaye hujampa njia mbadala ya kujikimu?” akauliza.

Amesema wakati wa utawala wa Rais wa Nne Uhuru Kenyatta, alileta Kazi Mtaani iliyookoa vijana wengi.

Kwa ujumla, amesema kwamba Kenya Kwanza inapata asilimia 30 sawa na gredi ya ‘D-‘.

  • Tags

You can share this post!

Kenya Lionesses kikaangioni dhidi ya Afrika Kusini

Wakulima wakesha ndani ya mashamba wezi wakivizia mazao

T L