• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Kindiki, Muturi walalama Uhuru hana shukurani

Kindiki, Muturi walalama Uhuru hana shukurani

NA GEORGE MUNENE

VIONGOZI wa Kenya Kwanza wikendi, walimkosoa Rais Uhuru Kenyatta, wakimtaja kama msaliti ambaye hana shukrani kwa kukosa kuunga mkono azma ya Naibu Rais William Ruto kuwania urais.

Seneta wa Tharaka-Nithi Kithure Kindiki na Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi (pichani), wakiwa kwa kampeni, Kaunti ya Kirinyaga, walisema inasikitisha kuwa Dkt Ruto alimuunga Rais chaguzi za 2013 na 2017 lakini sasa amemgeuka na kumwona kama hasimu wake.

“Rais Kenyatta alishinda uchaguzi mara mbili kwa sababu ya Ruto na sasa anamuunga mkono Raila Odinga. Hata hivyo, tunamwaambia ajiandae kuenda Ichaweri kwa sababu tutamlemea Bw Odinga debeni,” akasema Bw Kindiki.

Pia alimshutumu Rais kwa kuwahangaisha viongozi ambao walimsaidia kutwaa mamlaka ya nchi hasa baada ya kuonekana kutomakinikia Urais tena Mahakama ya Juu ilipofuta ushindi wake mnamo 2017.

“Baada ya kumsaidia alituondoa katika kamati za bunge na kutufukuza nje ya serikali yake. Sasa anatulazimishia Bw Odinga. Si haki, anafaa kutuacha tukumbatie mkondo wa kisiasa ambao tumeupenda,” akaongeza.

Naye Bw Muturi alidai kuwa Rais Kenyatta anatumia Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i na Katibu katika wizara hiyo Dkt Karanja Kibicho kuwahangaisha wandani wa Dkt Ruto na kumfanyia kampeni Bw Odinga.

  • Tags

You can share this post!

Wagombeaji elfu 14 kuanguka Agosti 9

Wawaniaji 3 washinda viti bila kupingwa na yeyote

T L