• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
Kiunjuri awaonya Ruto na Raila kuhusu wawaniaji

Kiunjuri awaonya Ruto na Raila kuhusu wawaniaji

Na CHARLES WANYORO

ALIYEKUWA Waziri wa Kilimo, Mwangi Kiunjuri, ametoa wito kwa Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kutowaidhinisha wagombeaji wakati wa uchaguzi mkuu ujao katika ngazi za mashinani.

Aliwataka kuwapa fursa wapigakura kuwachagua wagombeaji wanaowataka hasa katika eneo la Mlima Kenya.

Bw Kinjuri ambaye ni kiongozi wa chama cha The Service Party alisema wanasiasa na vyama vya kisiasa vyenye sura ya kitaifa hawafai kuamua viongozi wanaopaswa kuchaguliwa katika maeneo ya mashinani.

Akiongea katika kanisa la EAPC, Bw Kiunjuri alisema: “Ukija hapa kutuambia kuhusu Raila ama Ruto, tutakuambia tunawajua, sasa tueleze kuhusu sera zako,” alisema.

“Kwa mara ya kwanza hakutakuwa na msisimko wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu,” alisema kiongozi huyo.

You can share this post!

Jinsi ya kuandaa biriani ya nyama ya n’gombe

Boda atupwa nje kwa kutafuna muguka huku ibada ikiendelea

T L