• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
Mbunge wa Kesses hatarini kuangushwa na bodaboda

Mbunge wa Kesses hatarini kuangushwa na bodaboda

NA FRED KIBOR

MASHINDANO ya kisiasa nchini yanaamika kuwa mchezo ghali unaochezwa na matajiri pekee, watu wenye fedha na wanaoendesha magari ya kifahari.

Ili kudhibiti kiwango cha pesa ambacho wawaniaji wa nyadhifa tofauti wanafaa kutumia, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilichapisha viwango hivyo kwenye gazeti rasmi la serikali Agosti 2021.

Kwa mfano, katika Kaunti ya Uasin Gishu, mtu anayewania nafasi ya ubunge alilkuwa ameruhusiwa kutumia hadi Sh42 milioni kwenye kampeni zake, ingawa wabunge walitupilia mbali ilani hiyo baadaye.

Hata hivyo, mhudumu mmoja wa bodaboda katika eneobunge la Kesses, ameamua kutotamaushwa na masharti hayo makali, katika azima yake ya kumkabili mbunge wa sasa, Swarup Mishra.

Bw Felix Ruto, 29, maarufu kama ‘Hustler Mdogo’ ameamua kufanya kila awezalo kutozima ndoto yake.

Kwa kushirikiana na marafiki wake, Bw Rutto alifanikiwa kuchanga Sh125,000 kumsaidia kulipa ada ya uteuzi wa chama chake.

Bw Rutto analenga kuwashinda wawaniaji wengine watano kwenye mchujo wa chama cha UDA, utakaofanyika Aprili.

Bw Mishra amesema huenda akatetea kiti chake kama mwaniaji huru.

Miongoni mwa wale atakaokabiliana nao kwenye mchujo huo ni aliyekuwa Waziri wa Fedha katika kaunti hiyo, Bw Julius Rutto, aliyekuwa Spika wa Bunge la Kaunti, Isaac Terer, mfanyabiashara Joseph Kemboi, mbunge wa zamani wa eneo hilo James Bett na mtaalamu wa masuala ya mchanga, Bw Samuel Rono.

Tayari, Bw Rutto ameipamba pikipiki yake kwa rangi maalum huku akiitumia kufanyia kampeni katika sehemu tofauti eneo hilo.

Kinyume na washindani wake, hana magari yenye vipaza sauti kucheza ngoma kwa sauti za juu.

Badala yake, amekuwa akitumia pikipiki kufanyia kampeni kutoka nyumba moja hadi nyingine.

“Nina imani kumshinda Bw Mishra, ingawa amenishinda sana kiutajiri. Hatuwezi kulinganishwa hata kidogo,” akasema Bw Rutto kwenye mahojiano na ‘Taifa Leo’ mjini Eldoret.

Anasema alianza kudhihirisha uwezo wa kuongoza tangu utotoni, alipochaguliwa kuwa kiranja akiwa mwanafunzi katika Shule ya Msingi ya Kiptega.

Baadaye, alichaguliwa kuwa kiongozi wa wanafunzi wote shuleni humo.

Katika Chuo Kikuu cha Laikipia, alitoa mchango mkubwa alipohudumu kama mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi kutoka Kaskazini mwa Bonde la Ufa.

Hata hivyo, nusura ndoto yake ya kisiasa isambaratike mnamo 2020, baada ya wazee katika kijiji cha Kiptega kushangazwa sana na nia yake kuwa mbunge.

  • Tags

You can share this post!

Achani aponda wapinzani kuhusu maendeleo Kwale

Ashtakiwa kwa matusi mitandaoni

T L