• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 12:03 PM
Mtihani mgumu kwa Orengo akilenga ugavana Siaya

Mtihani mgumu kwa Orengo akilenga ugavana Siaya

NA CHARLES WASONGA

CHAMA cha ODM chake mgombeaji urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga kinakabiliwa na kibarua kikubwa katika kinyang’anyiro cha ugavana kutokana na hatua ya wagombeaji wawili Nicholas Gumbo na Charles Owino kuungana na kuhamia chama cha United Democratic Movement (UDM).

Wadadisi wanabashiri kuwa wawili hao watamtoa kijasho Seneta wa Siaya James Orengo ambaye anapigiwa upatu kupata tiketi ya ODM kuwania kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Bw Gumbo, ambaye ni mbunge wa zamani wa Rarienda, atawania ugavana huku Bw Owino akiwa mgombea mwenza wake kwa tiketi ya chama hicho ambacho ni mojawapo ya vyama tanzu katika muungano wa Azimio la Umoja.

UDM inaongozwa na Gavana wa Mandera Ali Roba.

Bw Owino, ambaye ni msemaji wa zamani wa polisi, amesema aligura ODM baada ya kung’amua kuwa chama hicho kinapanga kumkabidhi Bw Orengo tiketi ya moja kwa moja.

“Niliona dalili za mapema kwamba ODM ilikuwa inampendelea Bw Orengo ndiposa nikahama mnamo Machi 24, 2022 siku mbili kabla ya kukamilika

kwa makataa ya watu kujiunga na vyama vya kisiasa mnamo Machi 26, 2022” akasema Jumanne katika makao makuu ya UDM jijini Nairobi.

Naye Bw Gumbo, ambaye aliwahi kushikilia wadhifa wa mwenyekiti wa Kamati ya Uhasibu (PAC) anasema kuwa aligura chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga, kutokana na kile alichotaja kama “mivutano ya siasa za mashinani” katika kaunti ya Siaya.

Wawili, hata hivyo wanashikilia kuwa wataunga mkono ndoto ya Bw Odinga kuingia Ikulu “kwa hali na mali”.

“Nataka wakazi wa Siaya na taifa kwa ujumla kuelewa kuwa tumejiunga na UDM si kwa nia ya kuhujumu yeyote bali ni kuwapa wafuasi wetu nafasi ya kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao. Kujitokeza kwao kwa wingi ndiko kutamhakikishia Bw Odinga ushindi katika kinyang’anyiro cha urais,” Bw Gumbo.

Lakini mchanganuzi wa masuala ya kisiasa David Okello anasema kuwa chama cha ODM sasa kitalazimika kupanga mikakati mipya ya kushinda kiti cha ugavana wa Siaya baada ya hatua ya Mbw Gumbo na Owino.

“Sababu ni kwamba, japo seneta Orengo ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa, upungufu wake ni kwamba rekodi yake ya maendeleo haipendezi. Wapigakura eneo la Luo Nyanza siku hizi wamebadili mitazamo yao hivi kwamba wengi wao wameanza kuwachagua viongozi kwa misingi ya rekodi yao ya maendeleo wala si chama maarufu eneo hilo,” Dkt Okello ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Kulingana na msomi huyo, wapigakura wa kaunti ya Siaya walidhihirisha hilo katika uchaguzi mdogo wa eneo la Ugenya mnamo Aprili 28, 2019. Mgombeaji wa ODM Christopher Karan alishindwa na mbunge wa sasa David Ochieng’ ambaye aliwania kiti hicho kwa tiketi ya chama Movement for Democracy and Democracy (MDG).

  • Tags

You can share this post!

Kufeli kwa BBI pigo kwa Raila na Ruto

Mgombea mwenza wa ugavana Mombasa alivyo na usemi mkuu

T L