• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Muungano wa Kenya Kwanza waibuka na wawaniaji wake wa nyadhifa za uongozi bungeni

Muungano wa Kenya Kwanza waibuka na wawaniaji wake wa nyadhifa za uongozi bungeni

NA SAMMY WAWERU

MUUNGANO wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Rais William Ruto umeibuka na wawaniaji wake wa nyadhifa za uongozi bungeni.

Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa ndiye atakayewania wadhifa wa Kingozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa.

Bw Ichungwa ameteuliwa Jumamosi katika mkutano wa wajumbe wa mrengo huo tawala mjini Naivasha, Kaunti ya Nakuru.

Naye Seneta wa Kericho, Aaron Cheruiyot ameteuliwa kuwa ndiye atawania wadhifa wa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti.

Ichungwa atakuwa akisaidiwa na Owen Baya, ambaye ameteuliwa kama naibu wake, na Bw Cheruiyot, seneta wa Nakuru, Bi Tabitha Karanja.

Wakati huo huo, mbunge wa Mugirango Kusini, Silvanus Osoro ameteuliwa kiranja wa wengi bunge la kitaifa naibu wake akiwa Naomi Waqo.

Naye Seneta wa Kakamega, Dkt Boni Khalwale ameteuliwa kuwa Kiranja wa Seneti ambapo atakuwa akisaidiwa na Stephen Lelegwe kama naibu.

Aidha, Rais Ruto amesema wapinzani wao wakuu wa mrengo wa Azimio La Umoja-One Kenya wanapoteza muda kudai wao ndio wengi.

“Marafiki wetu (Azimio) wanapoteza muda wao kudai ndio wengi… Wao watachagua Viongozi wa Wachache,” amesema Rais Ruto.

Mnamo Septemba 8, 2022 kiongozi wa Ford-Kenya Moses Wetang’ula alichaguliwa na wabunge kuwa Spika Bunge la Kitaifa, naye aliyekuwa Gavana wa Kilifi akachaguliwa na maseneta kuwa Spika wa Seneti.

  • Tags

You can share this post!

Waiguru achaguliwa mwenyekiti wa Baraza la Magavana

Msipeleke tamaa bungeni, Raila aonya viongozi

T L