• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
Ndindi Nyoro asuta Jubilee kwa kutishia kumng’oa Ruto

Ndindi Nyoro asuta Jubilee kwa kutishia kumng’oa Ruto

NA LABAAN SHABAAN

MBUNGE wa Kiharu Ndindi Nyoro amepuuzilia mbali vitisho vya chama cha Jubilee akisema ni chama kidogo sana kujaribu kumbandua Rais William Ruto kutoka mamlakani.

Akizungumza katika ibada kanisani Mbuinjeru eneobunge la Runyenjes Kaunti ya Embu, Bw Nyoro aliwaka kuwa tukio la Jubilee kuwasilisha hoja ya kumbandua Rais halina msingi na mashiko yoyote.

“Hicho chama hata pale bungeni hakina Kinara (Mbunge Mteule Sabina Chege) kwa sababu alihama. Wataleta mswada wa kumbandua vipi?” alisema.

“Nawaambia kwa ukweli hawawezi kufaulu kwani hawana idadi na hawajui wanafanya ya nini,” akaongeza.

Kwa moto uo huo Bw Nyoro aliwataka viongozi wa Upinzani wakosoe serikali huku wakiwa na subira kuruhusu serikali ya Kenya Kwanza kutimiza mipango yake.

“Wewe (Uhuru Kenyatta) ulipewa nafasi ya kuwa Rais lakini yule ameingia (Rais Ruto) unamwekea mitego ya kuanguka,” alielekeza shutuma kwa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

Wakati uo huo, Mbunge wa Kiharu amewarai Wakenya kuwa na subira serikali ‘ikijizatiti’ kuwakomboa kutoka katika hali ngumu ya kiuchumi.

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula alikariri kauli ya Bw Nyoro akiomba Upinzani uvumilie serikali inapobuni mbinu ya kufufua uchumi.

Mrengo wa Chama cha Jubilee kinachoongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Ndaragwa Jeremiah Kioni umetisha kuwasilisha hoja ya kumng’atua ofisini Rais Ruto.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi wazungu weusi wanavyotesa ‘ushago’

Mama aponda wanawe kwa shoka na kutoweka

T L