• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 10:00 AM
Polisi wafuatilia madai dhidi ya mbunge wa Bahati

Polisi wafuatilia madai dhidi ya mbunge wa Bahati

NA MERCY KOSKEY

POLISI katika Kaunti ya Nakuru wanafuatilia kisa ambapo mwendeshaji kampeni wa Mbunge wa Bahati, Bw Kimani Ngunjiri, amedaiwa kuwashambulia watu wanaomfanyia kampeni mpinzani wake, Bi Irene Njoki, anayewania ubunge katika eneo hilo kwa tikiti ya Chama cha Jubilee.

Kamanda wa Polisi Bahati, Bw Samson Andanje, alisema maafisa wake wanamfuatilia mshukiwa mmoja ambaye yuko kwa kampeni ya Bw Ngunjiri.

“Kwa sasa tumemtambua mwendeshaji kampeni wa Bw Ngunjiri aliyemzaba kofi mwenzake wa kambi ya Bi Njoki wakati wa fujo za Jumamosi. Tunamuandama mshukiwa,” akasema Bw Andanje.

Bi Njoki mnamo Jumapili aliandamana na watu wawili wanaodaiwa kushambuliwa kuandikisha taarifa katika Kituo cha Polisi cha Bahati.

Akizungumza baada ya kuandikisha taarifa, dereva wa lori lililotumika kwa kampeni, Bw Simon Karanja, alidai mbunge huyo alianza kumpiga baada yake kukataa kuzima vipaza sauti.

Bi Njoki alidai kuwa lengo la Bw Ngunjiri ni kumpa vitisho ili kutowania nafasi hiyo na kuacha kufanya kampeni katika eneo hilo.

  • Tags

You can share this post!

Putin aombwa aketi na Zelensky wamalize vita

Agizo EACC ichunguze upya unyakuzi Vipingo

T L