• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:55 PM
Ruto afagia upinzani katika ngome yake

Ruto afagia upinzani katika ngome yake

NA TITUS OMINDE

WABUNGE wote waliochukuliwa kuwa waasi wa Naibu Rais William Ruto katika ngome yake ya Rift Valley walibwagwa kwenye uchaguzi wa Agosti 09, 2022.

Katika eneobunge la Nandi Hills kwenye Kaunti ya Nandi, Bw Benard Kitur (UDA), alimwangusha mbunge wa sasa Alfred Keter na kuvutia shangwe za aina yake.

“Leo ni ushindi mkubwa baada ya Kitur kuangusha simba Nandi,” alisema mmoja wa wafuasi wa Kitur.

Katika eneobunge la Kesses, Dkt Swarup Mishra alitemwa na Julius Ruto wa UDA.

Licha ya Dkt Mishra kuonyesha wenyeji ukarimu usio na kifani, alibanduliwa huku wapinzani wakimkejeli kwa msemo ‘sasa ni safari ya kuelekea Punjab’.

Mbunge wa Moiben, Bw Sila Tiren, hakusazwa kwani hata yeye alitimuliwa na Profesa Philips Bartoo wa UDA.

William Chepkut wa Ainabkoi alishindwa na mwandani wa Dkt Ruto, wakili Samuel Chepkonga.

Matokeo hayo yanaashiria ubabe wa Bw Ruto ambaye sasa atazingirwa na wabunge wa “Ndio Bwana!” hata wakitusiwa.

Amekuwa na kampeni ya kuzima wawaniaji huru akiwemo pia mgombea ugavana Uasin Gishu, Zedekiah Bundotich (Buzeki).

  • Tags

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Nancy Okware

Vurugu zatatiza shughuli ya kujumlisha kura Malindi

T L