• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 PM
Ruto ampokonya Keter nyama iliyokuwa mdomoni!

Ruto ampokonya Keter nyama iliyokuwa mdomoni!

NA LEONARD ONYANGO

WENGI walitabiri kuwa mbunge wa Nandi Hills Alfred Kiptoo Keter angevuta mkia katika kura za mchujo wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) chake Naibu wa Rais William Ruto.

Lakini waliokuwa wakitabiri hivyo wamegeuka kuwa manabii wa uongo kwani mbunge huyo machachari alipata ushindi mnono.

Lakini licha ushindi huo, uwezekano wa Keter kurejea Bungeni ni mfinyu baada ya kupokonywa nyama mdomoni.

Bodi ya kutatua mizozo ya UDA ilifutilia mbali ushindi wa Keter ikisema kuwa uchaguzi huo wa mchujo uligubikwa na udanganyifu.

Mara baada ya kutangazwa mshindi katika mchujo wa Jumanne, Bw Keter alinyimwa cheti cha uteuzi huku msimamizi wa uchaguzi akidai kwamba hakikuwa tayari.

Baada ya kunyimwa cheti, mwanafunzi huyo wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kati ya 2008 na 2012, aliagiza wafuasi wake wasiondoke kituoni hadi apewe cheti cha ushindi.

Kabla ya mchujo huo, wanasiasa wa UDA waliwasihi wakazi wa Nandi Hills kumkataa Bw Keter kutokana na tabia yake ya kutusi kinara wao.

Tangu 2017, Bw Keter amekuwa mkosoaji mkuu wa Naibu wa Rais na mnamo 2018 alitangaza kuwa ombi lake kuu lilikuwa Dkt Ruto asiwe rais wa tano wa Kenya.

Mnamo 2013, Bw Keter pia alitabiri kuwa Dkt Ruto angetemwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kumsaidia kuingia Ikulu – unabii uliogeuka kuwa wa kweli.

Makataa ya vyama vya kisiasa kufanya mchujo na kutatua mizozo yakiwa yamepita, uwezekano wa kurudia mchujo Nandi Hills ni finyu na kuna uwezekano Keter kuachwa akimeza mate.

  • Tags

You can share this post!

Walimu 22,000 kupata mafunzo ya gredi 6, asema Magoha

441 kukosa matokeo ya KCSE sababu ya udanganyifu

T L