• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 5:55 AM
Wito viongozi wa Mlima Kenya waungane kwa manufaa ya wenyeji na wakazi

Wito viongozi wa Mlima Kenya waungane kwa manufaa ya wenyeji na wakazi

NA LAWRENCE ONGARO

VIONGOZI kutoka Mlima Kenya wameshauriwa kuungana pamoja na kuelekea njia moja.

Mbunge wa Juja Bw George Koimburi alisema wakati umefika kwa viongozi hao kushirikiana hadi mwaka wa 2027.

Aliyasema hayo wakati wa sherehe za Mashujaa Dei zilizofanyika katika eneo la Ndarasha, Juja, Kaunti ya Kiambu.

Aliwashutumu wanaokaa kitako wakiona pombe haramu na dawa za kulevya zikiangamiza wengi katika eneo la Mlima Kenya.

“Viongozi wasiosaidia raia hawana faida yoyote,” alisema Bw Koimburi.

Alisema yeye atapambana na wanyakuzi wa mashamba ambao wamehangaisha wakazi wa eneo hilo.

“Mimi sitakaa kitako na kutazama wanyakuzi wa mashamba wakitawala eneo langu,” alisema Bw Koimburi.

Alisema atatenga Sh7.8 milioni kujenga shule ya upili katika eneo la Ndarasha.

Wakati wa sherehe hizo, mbunge huyo na wakuu wa serikali waliharibu bangi magunia 172 na kumwaga pombe haramu kiasi cha lita 2,000.

Kamishna wa Kaunti ya Kiambu Bw Joshua Nkatha aliwapa ilani walaghai wa mashamba katika eneo hilo akisema siku zao zinahesabiwa.

“Tumegundua ya kwamba kuna watu fulani ambao huandamana na wanunuzi wa mashamba wakidai kuna shamba la kuuzwa. Baadaye wao huwaua wanunuzi hao na kuwaacha hoi,” alisema kamishna huyo.

Alisema tayari serikali inawasaka na ikiwapata adhabu yao haitakuwa nyepesi.

“Kwa hivyo wawe chonjo,” akasema.

Alisema kwa muda wa mwezi mmoja, maafisa wa polisi wamewakamata watengenezaji pombe kadhaa na kuwapeleka mahakamani.

Alisema kwa huo mwezi mmoja katika mahakama za Kiambu, takriban Sh2.4 milioni za faini zimetozwa kutoka kwa watengenezaji wa pombe haramu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wakuu wengi wa serikali, na viongozi wa kisasa kutoka eneo hilo.

  • Tags

You can share this post!

Maseneta wataka DCI ichunguze uhusiano kati ya Pasta...

Maskini Simba! Afadhali Diamond Platnumz angejua Kizungu

T L