• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:50 AM
NGUVU ZA HOJA: Ahadi ya Waziri Amina ya kuunda Baraza la Kiswahili isiwe hewa tupu

NGUVU ZA HOJA: Ahadi ya Waziri Amina ya kuunda Baraza la Kiswahili isiwe hewa tupu

NA PROF IRIBE MWANGI

PROF. Kimani Njogu, Prof. Rayya Timammy, Prof. Mwenda Mbatiah, Prof. Clara Momanyi na Prof. John Kobia ni kati ya wasomi wengi walioomboleza kwa sauti kuhusu kutoundwa kwa Baraza la Taifa la Kiswahili (BATAKI).

Maombolezi hayo yalifanywa Alhamisi iliyopita wakati wa kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani.

Kilio chao kilianza asubuhi kwenye lango kuu la KICC na hatimaye kuendelea jioni kwenye Makavazi ya Kitaifa. Kilio hicho kiliongezwa sauti na Waziri wa Utalii na Wanyamapori Mhe. Najib Balala. Yalikuwa maadhimisho ya furaha na kilio kwa pamoja.

“Leo imekuwa siku ngumu sana kwangu, tatizo linalotajwa kuhusu Baraza linaanguka kisawasawa ofisini mwangu … kama ningekuwa na mahali pa kujificha, ningefanya hivyo … lakini Waziri ataongea,” alisema Katibu Mkuu anayesimamia Utamaduni na Turathi Bi. Josephta Mukobe.

Kwa muda mrefu, wasomi, wakereketwa na wapenzi wa Kiswahili wamekuwa wakiomba kuundwa kwa Baraza hilo ili liweze kusukuma na kuweka laini maswala ya Kiswahili.

Katika mkataba uliozindua Jumuiya ya Afrika Mashariki, swala la Baraza limeelekezwa wazi wazi.

Kiswahili ni lugha yenye majukumu muhimu kikatiba nchini: ni lugha aslia ya jamii fulani, ni lugha ya taifa na tatu ni lugha rasmi.

Siku hizi, lugha hii inatambulika sio tu katika bara la Afrika bali ulimwenguni kote.

Aliposimama kuzungumza akiwa Mgeni wa Heshima katika maadhimisho hayo, Waziri wa Michezo, Utamaduni na Turathi Balozi Amina Mohamed alieleza taifa kwamba atazindua Baraza katika muda usiopita mwezi mmoja.

Uundaji huo ulipitishwa na Baraza la Mawaziri mnamo 2018. Hii ni zawadi tunu kwa wapenzi wa Kiswahili.

  • Tags

You can share this post!

BITUGI MATUNDURA: Siku ya Kiswahili Duniani ina mawanda...

NGUVU ZA HOJA: Yapo matumaini ya kuundwa kwa Baraza la...

T L