• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 11:13 AM
Demu akubali mistari ya jamaa kwa sharti moja: “Utanilipa ada kila mwezi”

Demu akubali mistari ya jamaa kwa sharti moja: “Utanilipa ada kila mwezi”

GITHUNGURI, KIAMBU

NA TOBBIE WEKESA

Kimada katika mkahawa mmoja wa eneo hili alimuacha polo kwa mawazo tele kutokana na msimamo wake.

Walipokuwa wakijivinjari, polo alimuomba kidosho ampakulie asali yake lakini jibu lake lilimuacha hoi.

“Niko tayari kukupakulia mzinga ulambe asali yote lakini hayo yote yatafanyika iwapo utaniahidi kuwa sponsa wangu,” kidosho alieleza.

Inadaiwa polo alimuangalia kidosho kwa muda bila kusema neno.

“Mimi sipendi watu wa siku moja na kupotea. Utamu wa asali ni kuendelea kurina kila wakati,” kidosho alieleza.

Polo alimueleza kidosho kuwa anahitaji muda kufikiria kuhusu suala hilo.

“Mimi nipo. Una nambari yangu. Tunda nitakupa kila wakati utalihitaji,” kidosho aliapa.

Wakati huo huo, kizaaza kilizuka katika eneo la Mosoriot, Kaunti ya Uasin Gishu baada ya mama mkwe kumzomea vikali mkazamwana.

Inadaiwa mama mkwe alikasirishwa na hatua ya kipusa kukataa kutekeleza masharti ya mganga.

“Mganga alituambia tusichote maji katika kisima kimoja na mtu fulani. Wewe ndiwe huyo umekiuka,” mama mkwe alifoka.

Kipusa alidai kwamba masharti ya mganga hayakuwa na uhalisia wowote kwani hauhusiani na matatizo yaliyowapeleka huko.

“Jana nimekuona kanisani na uliambiwa mlango wa kanisa uuonee kwa ndoto. Shida yako ni gani,” kipusa alifokewa.

Duru zinasema kipusa aliapa kutofuata masharti hayo.

  • Tags

You can share this post!

Ruto aonywa kuhusu mpango wa kuwaondolea wageni viza

Murkomen aondolea Kenya Power lawama za mahangaiko ya JKIA

T L