• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 9:50 AM
Kisanga polo akilaumu kahaba kwa kumzima nguvu za kiume kiuganga kwenye lojing’i

Kisanga polo akilaumu kahaba kwa kumzima nguvu za kiume kiuganga kwenye lojing’i

NA MWANGI MUIRURI 

THIKA
KIZAAZAA kilizuka katika lojing’i ya mji huu polo alipotaka kurejeshewa Sh150, alizokuwa amelipa kahaba akimlaumu kwa kumzima nguvu za kiume kwa kutumia uganga.

“Mimi najijua vyema. Mimi sio mtu wa kusukumwa ili injini yangu ingurume. Mimi sio gari la kusukumwa. Iweje tukiingia kwa chumba nilikuwa sawa lakini tukielekea kuanza niko goigoi?” kalameni akazusha.

Polo na mwanamke huyo walikuwa wameafikiana kurushana roho kwa muda mfupi, short time, kwa lugha ya mtaani, kwa bei ya Sh150.

Hali kadhalika, jamaa alikuwa alipe Sh100 zaidi za lojing’i ili wajivinjari kwa chini ya dakika 10.

“Tulitoana kule nje, na tukielekea kupiga moyo pasi nilikuwa sawa. Hata nilikuwa naumwa kwa sababu ya makali…Tulipoingia chumbani, nilikuwa sawa. Punde tu nikielekea kubisha langoni nikamate mwelekeo, mlingoti ukadhoofika kwa kasi,” akalia.

Polo aliongeza kuwa mrembo huyo alimpapasa lakini badala ya kuamka tena, alizidi kulala bila matumaini hata ya kurejelewa na haja za mahaba.

“Huo ni nini ikiwa sio uchawi? Cha kukera mno, tuliskizana kwamba kazi ilikuwa nitimize haja yangu ya kujamiana. Mimi mtoto wa watu hata sijaonja chumvi na ninaambiwa kwamba pesa yangu imeisha. Nimelipia huduma gani? Ya kuonwa tu uchi uliozimwa makali kiuganga?” akateta.

Ilibidi meneja wa lojing’i hizo aingilie kati ambapo alimtaka mrembo huyo amrejeshee polo Sh70 za kumtuliza.

Ingawa alikataa, aliambiwa kuwa yeye alikuwa ameandaliwa mlo roho safi yeye akakosa hamu na wa kulaumiwa sio mwingine, bali ni yeye na jembe lake.

Hali ilifanywa kuwa ngumu wakati wateja wa kahaba huyo waliokuwa mahali hapo walimtetea wakisema huduma zake huwa za uhakika na zisizo za ubishi.

Polo alichukua Sh70 zake kama fidia ya masaibu na akatokea eneo hilo akinung’unika kwamba haki ya mnyonge duniani ni vigumu kuipata.

 

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Wanamazingira waingiwa na wasiwasi mikoko ikifa Kitangani

Rais Ruto azindua pikipiki za umeme mjini Mombasa

T L