• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 7:22 PM
Paka mweusi amzuia jamaa aliyejaribu kuondoka dukani bila kulipia bidhaa

Paka mweusi amzuia jamaa aliyejaribu kuondoka dukani bila kulipia bidhaa

NA JANET KAVUNGA

MALINDI MJINI

KULITOKEA kioja katika duka moja mjini hapa jombi aliyetaka kuhepa bila kulipia bidhaa alipozuiwa kuondoka na paka mmoja mweusi.

Inasemekana kulikuwa na wateja wengi katika duka hilo na muuzaji akawa na shughuli nyingi kuwahudumia.

Jamaa alikabidhiwa bidhaa alizoitisha na alipokuwa akizipakia, mwenye duka alianza kuwahudumia wateja wengine na jombi akaamua kutumia fursa hiyo kuchomoka bila kulipia.

Hata hivyo, hakuwa na bahati kwa kuwa paka mmoja mkubwa mweusi alimzuia mlangoni na kutoa mlio uliowafanya wateja kushtuka.

Mwenye duka aligundua jamaa hakuwa amelipia bidhaa na akamuonya.

“Bwana we, hapa huwezi kuiba au kuondoka bila kulipa. Leta pesa,” mwenye duka alimwambia jamaa na alipolipia bidhaa zake, paka akamruhusu kuondoka.

  • Tags

You can share this post!

AMINI USIAMINI: Ndege anayefahamika kama Pelegrine falcon...

Leicester City waajiri kocha Enzo Maresca

T L