• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 11:13 AM
Polisi atapika baada ya kunusa vidole vya mshukiwa wa bangi

Polisi atapika baada ya kunusa vidole vya mshukiwa wa bangi

NA MWANGI MUIRURI

MARAGUA, MURANG’A

AFISA wa polisi alitapika aliponusa vidole vya kijana wa umri wa miaka 23 kutoka Kaunti ya Murang’a akimshuku kuwa ni mvuta bangi.

Kisanga hicho kilitokea Jumatatu usiku wiki hii na afisa alipohisi harufu mbaya ya mtu aliyejishika kwa makalio machafu, alimzaba kijana huyo kofi ya shavu.

Kijana wa kijiji cha Maica ma Thi aliambia meza ya dondoo kwamba mwendo wa saa tatu usiku katika mji wa Maragua ndipo kisa hicho kilimpata.

“Alikuwa amekaa kwa kichochoro fulani akila gumzo na wenzake wakisubiri saa tano ya usiku kutinga ndipo waende nyumbani. Walikuwa vijana watano,” akasema mdokezi.

Aliongeza kwamba maafisa watatu wa polisi waliingia katika kichochoro hicho cha mtaa wa Mathare na wakawaagiza wasimame huku wakimulikwa kwa miale mikali ya mwangaza wa tochi.

“Afisa mmoja aliwaamrisha wanyooshe mikono yao mbele na akaanza kunusa vidole. Kijana wa kwanza alikamatwa kwa msingi kwamba vidole hivyo vyake vilikuwa na harufu ya bangi,” akasema.

Wa pili na wa tatu pia walisemekana walikuwa wakinuka bangu “na ndipo kijana huyo aligundua kwamba utukutu ndio tu ungemwokoa”.

Mdokezi anasema kijana aliingiza viganja vya mikono ndani ya long’i yake na akajikunakuna kwa makalio yake ili vidole vinuswe.

“Afisa huyo aliponusa akapandwa na hasira kuu ghafla. Alimgonga kofi akaona vimulimuli. Hata hawakukamatwa kwa kuwa polisi wengine waliangua wakati wa kuwanusa vijana alienda kando kutapika,” akasema mdokezi.

Ni hatia kwa afisa wa polisi kushambulia raia.

“Iwapo kijana huyo angelalamika rasmi katika kituo cha polisi ninaweza nikamsaidia kupata haki yake. Lakini pia nimearifiwa kwamba walikokuwa wamekaa hao vijana kuliokotwa misokoto mitatu ya bangi,” akasema mkubwa wa afisa aliyetapika.

Mkubwa huyo alikiri kwamba mbinu ya kunusa vidole vya washukiwa ili kubaini kana kwamba kuna ushahidi wa uvutaji bangi imeingiwa na kila aina ya ujeuri “kujikuna ndani ya makalio ikiwa ni mmojawapo wa ujeuri huo”.

Mkubwa huyo alikoma kuitumia mbinu hiyo baada ya kuathirika mara kadhaa.

  • Tags

You can share this post!

Siri ya kujinasia wateja ni majina tamutamu ya boti

Ghasia zatatiza biashara nchini

T L