• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 8:09 PM
Polo alia kama senge lojing’i Murang’a baada ya kumeza kukumanga kusisimua mahaba

Polo alia kama senge lojing’i Murang’a baada ya kumeza kukumanga kusisimua mahaba

NA MWANGI MUIRURIĀ 

MWANAMUME aliyekuwa amemeza kukumanga katika mji wa Murang’a alishangaza wateja wenzake katika lojing’I, alipoanza kulia kama senge.

Alikiri kuwa alikuwa amemeza tembe mbili za miligramu 100 kwa kila moja, lakini kipusa aliyekuwa apige moyo pasi naye hakufika.

“Huyo mwanamume aliumia na ilibidi nikimbie hadi mtaa wa Biashara kusaka kahaba wa kulipwa ili aokolee hali…Sema mlingoti kusimama wima kama ile miti ya Lebanoni…Usiwahi kujaribu hivyo tena, nakuonya,” akasema bawabu wa lojing’i hiyo.

Kalameni alisema kwamba huwa anameza tembe hizo ili kulima shamba kadri ya pesa zake.

“Kwa kuwa mahaba ni pesa siku hizi, niligharamia na lazima nami nirarue shamba kwa kiwango tosha. Pesa kupata ni jasho na lazima kipusa aniridhishe,” akasema.

Wateja walisema kwamba waliamshwa na kelele za polo huyo mwendo wa saa sita na kuamka kuchungulia kulikoni, wakamwona jamaa akiwa uchi wa mnyama huku jembe lake likijichomoza mbele kama mkuki.

“Alikuwa akitoa sauti za kulalama, huku akiomba asaidiwe kabla ya mishipa ya jembe ipasuke. Alisema angegharamia afueni na ndipo bawabu akarukia mwanya huo wa kupata pato la haraka,” akasema mdokezi.

Ndipo polo alimpa bawabu huyo Sh3, 000 ajipange nazo kumlipa kipusa mbadala na pia ajitengee malipo.

“Nilimwona Mungu na macho haya yangu mawili kwa kuwa nilipata Sh2, 000 na nikalipa kipusa Sh1, 000. Nilituliza hali na nikitoka kazini asubuhi ya Agosti 20, 2023 hali ilikuwa shwari,” akasema bawabu mjuzi wetu.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Gachagua: Ninaweza kufundisha Kiingereza katika Shule ya...

Stivo Simple Boy ajinyakulia kipusa kitu kipya, Wanja Kihii

T L