• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:55 PM
Polo atoweka kazini ghafla kukwepa bosi wa kumtupia mistari kila mara

Polo atoweka kazini ghafla kukwepa bosi wa kumtupia mistari kila mara

NA JANET KAVUNGA

MTWAPA, KILIFI

BAROBARO mmoja aliamua kususia kazi ili kuepuka majaribu baada ya mdosi wake mwanadada kumrushia chambo.

Jamaa alisema mara si moja bosi wake katika hoteli ya hapa alimuita katika ofisi na kumnyanyasa kimapenzi kwa kumpapasa, kumkumbatia na kumpiga mabusu bila hiari yake.

Aliungama kuwa bosi alitisha kumfuta kazi alipokataa mwaliko waende date akamlishe raha.

“Ninachelea kwenda kazini kwa kuwa vitendo vya bosi wangu vinanisinya. Siwezi kurushana roho naye ilhali ni mke wa mtu,” akatanguliza.

“Badala yake kunipiga kalamu kwa kukataa mistari yake au kuikubali na nizini, heri niache kazi na niwe na amani yangu,” jamaa aliambia wenzake walipomuuliza sababu ya kukosa kufika kazini.

  • Tags

You can share this post!

Kwa mara ya kwanza akina mama wa Kibajuni kisiwani Pate...

UDA Mlima Kenya wadai vyeo vya juu

T L