• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
Warembo waangushana kuona kiongozi wa vijana akiwa na gari

Warembo waangushana kuona kiongozi wa vijana akiwa na gari

Na LEAH MAKENA

SOUTH C, NAIROBI

WAREMBO katika kanisa la hapa walishangaza washiriki walipoangushana chini wakipigania gari la kiongozi wa vijana.

Duru zasema kuwa polo mwenye gari alipata kazi yenye mshahara mnono na kufanya warembo wengi kuanza kummezea mate.

Siku ya tukio, warembo hao walihudhuria ibada kama kawaida ila wakashangaza kung’ang’ania kiti cha mbele cha gari la polo punde tu ibada ilipokamilika.

Vuta nikuvute kati ya warembo hao ilianza waliporushiana cheche za matusi na kupigana kila mmoja akidai polo alikuwa chali wake.

Ilibidi akina mama waingilie kati kutenganisha wawili hao na kuwakaripia vikali.

“Mbona mnajiaibisha kwenye uwanja wa kanisa? Kama mnataka drama tokeni nje, tumechoka na vituko vyenu”.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Bodi iziondoe dawa hatari hospitalini

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuoka mkate mtamu wa siagi

T L