• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 PM
Azerbaijan yaitaka Armenia kukomesha kampuni zinazochafua Mto Okhchuchay

Azerbaijan yaitaka Armenia kukomesha kampuni zinazochafua Mto Okhchuchay

Mtafiti akichukua sampuli ya maji katika Mto Okhchuchay ambao rangi yake imebadilika na kuwa ya manjano kutokana na kemikali. PICHA/ HISANI

NA MASHIRIKA

KAMPUNI mbili nchini Armenia ndizo zinahusika na uchafuzi wa hali ya juu wa Mto Okhchuchay, mwanadiplomasia kutoka Azerbaijan amesema.

Ruslan Nasibov, afisa wa masuala ya kigeni katika afisi ya ubalozi ya Azerbaijan jijini Addis Ababa, Ethiopia, amesema said tatizo kubwa la kimazingira na kiafya liko njiani katika nchi hiyo kutokana na uhafuzi wa kiholela wa Mto Okhchuchay.

“Tunakerwa mno na athari za kimazingira na kiafya kutokana na uchafuzi wa unaoendelea katika Mto Okhchuchay unaoendeshwa na kampuni mbili kutoka Armenia,” alisema.

Bw Nasibov alisema mto huo ambao unatoka Armenia hadi Azerbaijan unachafuliwa na kampuni mbili za kimataifa – Zangezur Copper Molybdenum Combine na Kapan Mining & Processing Plant, zilizo nchini Armenia.

“Mto huo umechagfuliwa sana na uchafu unatotupwa humo ndani kutoka kwa viwanda vya kampuni hizi na sasa ni tisho kwa Maisha ya wananchi wa Azerbaijan,” alisema balozi huyo.

Alifichua kuwa utafiti uliofanywa kati ya Januari na Machi mwaka huu unaonyesha kuwa kiwango cha juu cha madini hatari kama copper, molybdenum, magnanes, iron, zinc na chromium kimeingia katika maji yam to huo.

“Tulichogundua ni kuwa kiwango cha uchafuzi katika mto huo kilikuwa juu ikilinganishwa na mito mingine inayotoka mataifa jirani,” alisema.

Aliongeza kuwa kuchafuliwa kwa maji ya mto huo kutaumiza wanyama wa majini na kuhatarisha Maisha ya maelfu ya watu wanaotumia maji hayo chafu na kumbukizwa magonjwa.

Asilimia 70 ya maji yote nchini Azerbaijan hutokana na mito inayoingia nchini humo kutoka mataifa Jirani, ukiwemo Mto Okhchuchay.

Bw Nasibov alisema maji kutoka mto huo hutumika sana kwa kunywa na kunyunyizia mimea. Uchafuzi huo wa maji yanayotumiwa kwa shughuli za nyumbani na kilimo unaweza kuzua athari mbaya kwa wakazi.

Kulingana na tafiti kadhaa, mwanadiplomasia huyo alisema, rangi yam to huo imebadilika na kuwa ya manjano ya aside huku samaki wengi wakiuawa kutokana na kiwango kikubwa cha kemikali.

“Kutokana na hili, tunaomba jamii ya kimataifa kuingilia kati suala hili ambalo Armenia inahusika, wakiwemo Waafrika,” alisema.

Alisema kampuni husika zimedinda kufuata kanuni za kimataifa kuhusu mazingira kwa kutupa taka kwenye mto huo bila kujali huku Armenia ikifumbia macho sual hilo ikijua ni kitendo kisichokubalika kwani kinahatarish amaisha ya watu wa Azerbaijan nae neo la Caucus kwa jumla.

“Hili si jambo tu la watu wa Azerbaijan lakini kwa kila mtu anayejali Maisha ya wanadamu katika masuala ya mazingira na afya duniani wakiwemo wale wanaoishi Afrika,” alisema mwanadiplomasia huyo.

Bw Nasibov alisema nchi yake inaamini kuwa maji yanafaa kuwa jambo la ushirikiano bali si mafarakano, akiongeza kuwa wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha kuwa Makubaliano ya Helsinki kuhusu Maji ya Mipakani yametiwa Saini na kila taifa husika.

Alisema Armenia bado haijatia saini mkataba huo ulioasisiwa mwaka 1992 nchini Finland kwa lengo la kuimarisha mikakati ya kitaifa na ushirikiano wa kimataifa wa kulinda maji ya mipakani na yale ya nchini.

  • Tags

You can share this post!

Yaibuka Mfanyabiashara wa Sudan kusini raia wa Kenya...

Uteuzi wa Chiloba ni njama ya kuboronga uchaguzi 2022...