• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 5:29 PM
Dhambi za zamani: Kidero ashtakiwa kwa ufujaji pesa miaka 9 iliyopita

Dhambi za zamani: Kidero ashtakiwa kwa ufujaji pesa miaka 9 iliyopita

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero na mbunge wa zamani wa Embakasi ya Kati John Ndirangu Kariuki walishtakiwa jana kwa ubadhirifu wa Sh58 milioni.

Dkt Kidero aliyekuwa miongoni mwa manaibu mawaziri 50 walioteuliwa na Rais William Ruto kabla ya kufutwa kazi na mahakama kuu alishtakiwa upya mbele ya hakimu mkuu Bw Felix Kombo katika mahakama ya kuamua kesi za ufisadi.

Dkt Kidero, Bw Kariuki, wahasibu sita na wakurugenzi wawili wa kampuni ya The Cups Limited John Ngari Wainaina na George Wainaina Njogu walikanusha mashtaka 15.

Dkt Kidero alikabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh14.4milioni pesa za umma.

Hakimu alifahamishwa pesa hizi zilikuwa sehemu ya Sh58 milioni zilizokuwa zimelipwa kampuni ya marehemu wakili Steven Kariuki Mburu 2014.

Dkt Kidero pia alishtakiwa kujitajirisha na pesa alizojua zimepatikana kwa njia ya ufisadi.

Bw Kariuki aliyekuwa Meya wa Jiji la Nairobi alikabiliwa na shtaka la kutia kibindoni Sh8.9 milioni kutokana na kitita  hicho cha Sh58 milioni kilichokuwa kimeporwa kaunti ya Nairobi Januari 2014.

Hakimu alifahamiwa Sh17 milioni zilitumika kununua ardhi na Sh2 milioni kutumika kulipia deni la aliyekuwa diwani Mutunga Mutungi.

Hakimu alifahamishwa waliokuwa wahasibu sita katika serikali ya Dkt Kidero walishiriki katika ubadhirifu huo wa fedha za umma.

  • Tags

You can share this post!

Daktari aliyeshtakiwa kumnajisi msichana aachiliwa kwa...

Mwalimu afariki siku chache kabla ya kuanza kazi...

T L