• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
DPP aagizwa awape ushahidi washukiwa wa ulaghai wa dhahabu

DPP aagizwa awape ushahidi washukiwa wa ulaghai wa dhahabu

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA imempa siku 13 Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya umma (DPP) Noordin Haji kuwapa nakala za ushahidi washukiwa watatu wa kashfa ya dhahabu.

Hakimu mkuu mahakama ya Milimani Susan Shitubi alitoa agizo hilo baada ya raia wa Congo Mansoni Didier na Wakenya wawili Partick Ngare Muchina na Kelvin Mwaura Ngotho kumweleza hawajakabidhiwa ushahidi na DPP kuwawezesha kuandaa tetezi zao.

Didier, Muchina na Ngotho wanakabiliwa na shtaka la kumlaghai Bw Sadegh Sadeghain Abolfazi Sh64 milioni wakidai walikuwa na uwezo wa kumuuzia kilo 60 za dhahabu.

Bi Shitubi alimwamuru DPP awakabidhi ushahidi watatu hao kabla ya Mei 18 kesi itakapoanza kusikizwa.

Kesi hiyo ilikuwa imeorodheshwa kusikizwa Alhamisi lakini “DPP alichelewa kuwapa washtakiwa nakala za mashahidi.”

Washtakiwa walilalamika kwamba hawakupewa nakala za ushahidi na muda wa kutosha kujiandaa kuwakabili mashahidi.

Watatu hao walikabiliwa na shtaka la kumlaghai Abolfazi mamilioni hayo wakidai watamwuzia dhahabu kilo 60 na kumsafirishia hadi Dubai.

  • Tags

You can share this post!

Kila akiwa uwanjani, kijana Ryan Ochieng hujitahidi kuiga...

KWPL: Vita vya Gaspo Women na Vihiga Queens kutwaa ubingwa...

T L