• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Hisia mseto bei ya gesi ikishuka katika maeneo tofauti

Hisia mseto bei ya gesi ikishuka katika maeneo tofauti

NA RICHARD MAOSI

Hisia mseto zimeibuliwa nchini baadhi ya miji ikishuhudia kupungua kwa bei ya gesi.

Hili linajiri siku chache baada ya wananchi kushinikiza serikali iweke mipango ya kuteremsha bei ya bidhaa muhimu mojawapo ikiwa ni gesi ya kupikia.

Taifa Dijitali ilizuru eneo la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu ambapo tulibaini kilo sita ya gesi inauzwa kati ya Sh1,100-1,200, kinyume na bei ya awali 1,300.

Aidha,  kilo 13 imeshuka kutoka Sh2,600 hadi kati ya Sh2,200 na 2,300.

Albert Ndegwa, muuzaji gesi kutoka Thogoto viungani mwa mji wa Kikuyu anasema ni hatua ambayo imepokelewa kwa mikono miwili, akipendekeza hatua kama hiyo ifanyike kwa mafuta.

“Mjini Nakuru kilo sita ya gesi imesalia kuwa Sh1,300, huku kilo kumi na tatu ikiuzwa kati ya Sh2,400 hadi 2,500,”hii ni kulingana na Yusuf Ali, muuzaji  kutoka mtaa wa St Marys  Nakuru.

Ali anasema angetamani kufikiwa na gesi ya bei nafuu, ikizingatiwa kuwa baadhi ya wanunuzi wake wamegeukia makaa tangu gesi zipande.

Aliongezea kuwa bei ya mtungi wa gesi ndio imeteremka kutoka Sh5,000 hadi Sh3,500.

Kwingineko, mjini Eldoret, kilo sita imebakia Sh1,200 huku mtungi wa kilo 13 ya gesi ukiuzwa kati ya Sh2,300-2,400.

  • Tags

You can share this post!

Brown Mauzo atangaza kutengana na Vera Sidika

Wanagofu 280 kuwania taji la Legendary uwanjani Ruiru

T L