• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 11:37 AM
Mfanyabiashara ashtakiwa kwa wizi wa mbolea ya Sh6 milioni

Mfanyabiashara ashtakiwa kwa wizi wa mbolea ya Sh6 milioni

NA RICHARD MUNGUTI

MFANYABIASHARA ameshtakiwa kwa kula njama za kuiba mbolea kiasi kinachofika magunia 5,000 yenye thamani ya Sh27.8 milioni ikisafirishwa kutoka Mombasa hadi North Rift.

Eric Kiarie Ng’ang’a alishtakiwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhubi.

Alikanusha mashtaka matatu ya kula njama za kuiba magunia 1,120 ya mbolea yenye thamani ya Sh6 milioni.

Hakimu alifahamishwa na kiongozi wa mashtaka Bi Virginia Kariuki kwamba kesi dhidi ya Ng’ang’a itaunganishwa na nyingine dhidi ya washukiwa wengine saba.

Saba hao ni Joseph Wamakau, Stanley Mumo, Martin Kioko, Beatrice Mwikali, Fredrick Gateri, Joseph Matheka na Anthony Kimuyu.

Ng’ang’a alikana kwamba kati ya Mach1 21 na Aprili 27, 2023 mahala pasipojulikana akiwa na wenzake, walikula njama za kuiba magunia 5,000 ya mbolea ya thamani ya Sh27,830,000 mali ya serikali.

Mbolea hiyo ilikuwa imeingizwa nchini kutoka ng’ambo.

Ng’ang’a alikabiliwa na mashtaka mengine ya kuiba mbolea magunia 1,120 ya thamani ya Sh6,160,000.

Mbolea hiyo ilikuwa inasafirishwa kutoka bandari ya Mombasa kupelekwa kwenye mabohari ya nafaka na mazao yaliyoko Kamwosor.

Mshukiwa mwingine alishtakiwa kuiba mbolea kiasi cha magunia 560 na yenye thamani ya Sh3,080,000.

Kwa ujumla mbolea ya thamani ya Sh9m iliibwa.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh600,000.

Kesi itaunganishwa na hiyo ya washtakiwa saba mnamo Juni 13, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Wito watafiti washirikiane na idara za afya kuongoza...

AFC Leopards yapokonya Mukangula na Thiong’o majukumu ya...

T L