• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 9:55 AM
Mradi wa mabohari wa The Link kusaidia kuimarisha uchumi

Mradi wa mabohari wa The Link kusaidia kuimarisha uchumi

NA LAWRENCE ONGARO

KUNA haja ya kujenga mabohari ya kuhifadhi bidhaa hasa kunufaisha wakazi wa Kaunti ya Kiambu na maeneo jirani.

Tatu City, Chandaria Properties, M & T Construction na Steel Structure wamezindua mradi wa kujenga mabohari unaofahamika kama The Link, na mabohari hayo yatatumika kuhifadhi bidhaa za kila aina.

Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na washika dau tofauti mnamo Jumanne katika ardhi ya Tatu City.

“Tuna imani kuwa mradi huu wa kuzindua mabohari katika eneo hili ni muhimu kwa sababu yatatumika kuhifadhi bidhaa tofauti,” alisema Bw David Karimi ambaye ni naibu meneja wa ujenzi wa mradi huo.

Alisema mradi huo utaendelea kwa muda wa miezi 11 kabla ya kukamilika.

Alisema ana imani kwamba mradi huo utawavutia wajasiriamali kutoka nchi za nje kuja kuhifadhi bidhaa zao hapo kabla ya kuzisafirisha kwingineko.

Mwenyekiti wa mamlaka ya kiuchumi inayofahamika kama Special Economic Zone Bw Fred Muteti alisema mradi huo wa The Link una umuhimu mkubwa kwa sababu utaunganisha uchumi wa Kenya na maeneo mengine kwa kiwango cha asilimia 98.

“Sisi tuko tayari kushirikiana na wawekezaji kutoka popote pale ili kuinua uchumi wetu kwa kiwango cha juu,” alisema Bw Muteti.

Waziri wa Utalii, Biashara na Viwanda katika Serikali ya kaunti ya Kiambu Bi Nancy Gichung’wa, alisema wako tayari kushirikiana na Tatu City kwa sababu wanatekeleza miradi yao katika ardhi ya Kaunti ya Kiambu.

Alisema mradi huo ukikamilika utakuwa muhimu kwa sababu Kiambu inapakana na jiji kuu la Nairobi na pia viwanja vya ndege viko karibu na eneo hilo.

“Tunafurahia mradi huu kwa sababu wakulima wetu watapata fursa ya kuhifadhi bidhaa zao hapa kwa mabohari hayo kabla ya kuziuza bidhaa hizo kwingineko,” alisema Bi Gichung’wa.

Alisema vijana wengi watanufaika na ajira ambazo zimekuwa changamoto kwa wengi.

Tatu City imehifadhi kampuni tofauti zipatazo 75, huku ikiwa imeajiri zaidi ya wafanyakazi wapatao 9,000.

Wakati huo pia kuna shule za msingi na za upili zikiwa na idadi ya wanafunzi wapatao 4,500.

Lengo kuu la wakuu wa miradi ya aina hiyo ni kuinua hali ya uchumi na kuinua maisha ya wananchi huku majumba ya kifahari yakijengwa kwa wateja kutoka nje kuyanunua.

  • Tags

You can share this post!

Wito wa utangamano na amani Rais Ruto akizuru Lamu

Afueni wakazi wa Chepkitale wakiahidiwa kituo cha polisi

T L