• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 5:55 AM
Mtundu Sasha Obama apigwa picha akivuta bangi

Mtundu Sasha Obama apigwa picha akivuta bangi

NA RICHARD MAOSI

Sasha Obama, mwanawe Rais wa 44 wa Marekani Barack Obama kwa mara nyingine ameonyesha utundu wake mitandaoni baada ya kunaswa na wapigapicha wa paparazzi akivuta bangi akiwa amevalia bikini.

Licha ya kwamba Sasha alivalia sketi ndefu, sehemu kubwa ya mwili wake ilibakia wazi na miguuni kavalia champali.

Hili linajiri baada ya kuhudhuria tamasha la Siku ya Leba lililofanyika katika Jiji la Los Angeles, jimbo la California.

Ikumbukwe kwamba sio mara ya kwanza Sasha, 22, ambaye ni kitindamimba wa Obama kuonekana akikata kiu.

Katika picha tata zilizotundikwa mitandaoni, Sasha, bila kusita anaonekana akipokezana sigara ndefu na marafiki zake wawili kisha wakaanza kupandisha stimu.

Inawezekana ameiga tabia hii kutoka kwa babake mzazi ambaye wakati mmoja amewahi kuungama awali alikuwa akivuta hadi sigara 10 kwa siku moja.

Sasha akiwa na babake, Rais Obama miaka ya awali. Picha|Maktaba

Obama alianza kuvuta sigara akiwa mdogo ila alimwahidi mkewe Michelle Obama kuwa angeachana na uraibu huo kabla ya kujiunga na kinyanganyiro cha kuwania urais mnamo 2008.

Bw Obama aliweka historia kwa kuwa Rais wa kwanza mweusi kuongoza Marekani na ana mizizi yake nchini Kenya katika kijiji cha Kogelo, Nyang’oma, Kaunti ya Siaya.

Mara nyingi Sasha na dadake mkubwa, Malia huonekana wakifurahia maisha ikiwa ni baada ya kupata uhuru walipohitimu na Shahada ya Elimu ya Jamii kutoka Chuo Kikuu Cha Southern California Mei 2023.

  • Tags

You can share this post!

EACC yakataa kumrudishia Oparanya Sh2m ikisema inazipiga...

Dereva wa teksi aliyekula Sh40,000 za karao ajutia kitendo...

T L