• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:55 PM
Mume na mkewe katika kesi ya unyakuzi wa ardhi Lavington waachiliwa bila kushtakiwa

Mume na mkewe katika kesi ya unyakuzi wa ardhi Lavington waachiliwa bila kushtakiwa

Na RICHARD MUNGUTI

MTU na mkewe wanaodaiwa wamenyakua jumba la kifahari mtaani Lavington Nairobi walifikishwa kortini Agosti 21, 2023 lakini hawakushtakiwa.

Mahesh Kumar Bhatti na mkewe Anita Bhatti walifikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina lakini “waliondoka bila ya kushtakiwa.”

Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kwa kutoshtakiwa kwa Mahesh na Anita licha ya cheche kali kuzuka kuhusu umiliki wa jumba hilo.

Mmiliki wa ardhi na jumba hilo Bw Munir Ahmed Chowdhary,75 pamoja na mkewe wako nchini Uingereza wanapoendelea kupokea matibabu.

Baada ya Mahesh na Anita kuondoka kortini bila kusomewa mashtaka licha ya hakikisho kutoka kwa afisa wa idara ya uchunguzi wa uhalifu (DCI), wakili Moses Mabeya na Bashir Abdulrehman (ajenti anayetunza mali ya Munir) waliambia wanahabari wamepigwa na butwaa.

“Hatujui kinachoendelea. Mahesh na Anita wamekuwa hapa kortini na wameondoka tu pasi na kusomewa mashtaka,”Mabeya aliambia wanahabari.

Wakili huyo alisema hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kwa hakimu kwa kutoshtakiwa kwa wawili hao licha ya hakikisho kutoka kwa DCI na DPP.

Hata hivyo kuna kesi iliyowasilishwa katika mahakama kuu na Mahesh na Anita wakiomba watangazwe kuwa wamiliki halisi wa jumba na ardhi ambapo imejengwa wakidai waliinunua 1996 na wameishi mle bila bughudha.

Kwa upande wake Munir amesem alinunua uwanja ambapo jumba hilo limejengwa 1977. Amemiliki ardhi na jumba hilo kwa zaidi ya miaka 50.

  • Tags

You can share this post!

Kamati kuchunguza ikiwa kuna madhara Worldcoin kumulika...

Familia yataka maswali yajibiwe kuhusu mauaji ya jamaa yao

T L