• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Naibu Spika ataka polisi sasa waanze kuvalia kamera mwilini kurekodi matukio

Naibu Spika ataka polisi sasa waanze kuvalia kamera mwilini kurekodi matukio

NA NYABOGA KIAGE

Naibu wa Spika katika Bunge la Kitaifa Bi Gladys Boss Shollei anataka polisi waanze kuwekewa kamera mwilini kila wakati.

Bi Shollei alisema kuwa kamera hizo zitasaidia pakubwa kupambana na ufisadi nchini na kuhakikisha kuwa askari wanafuata sheria wakati wote.

“Kila askari anafaa kuvalia kamera mwilini kwa kufanya hivyo itasaidia pakubwa kupambana na ufisadi nchini,” Bi Shollei alisema.

Haya yanajiri wiki chache baada ya polisi kusolewa kwa kutumia nguvu kupitia kiasi walipokuwa wakipambana na waandamanaji wanaoegemea upande wa upinzani.

Kulingana na tume ya kutetea haki za binadamu, idadi ya watu ambao waliuawa na pia kuumizwa wakati wa maandamano hayo ilikuwa kubwa huku wakilinganisha visa hivyo na vitendo vya kigaidi.

Wakati maandamano hayo yalikuwa yamepamba moto, vifo kadhaa viliripotiwa ikiwa ni pamoja na watu 10 kupigwa risasi na polisi wiki iliyotangulia.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KHRC), ilisema “kulikuwa na mtindo wa kutatiza kuonyesha kwamba vitendo vya [polisi] na utumiaji nguvu wa mauaji vilipangwa”.

Hakuna idadi rasmi ya watu ambao waliaga dunia lakini tume ya Amnesty International inasema kuwa polisi waliwaua watu wasiopungua 30 tangu Machi.

Tume hizo za kutetea haki za binadamu zinasema kuwa askari waliokuwa wakipambana na waandamanaji kwenye kaunti za Magharibi, Kisumu na Migori walionekana kutekeleza amri ya kuua.

Hata hivyo, Rais William Ruto amekuwa akiwapongeza polisi kwa kufanya kazi nzuri walipokuwa walipambana na waandamanaji hao.

“Nawapongeza polisi kwa kusimama kidete, kwa kuhakikisha amani inakuwepo na kuhakikisha wahalifu wote wanachukuliwa hatua,” Rais Ruto alisema.

Katika kisa kingine kilichofanyika eneo la Mathare, askari aliyekuwa amevalia kiraia na kujifanya mwanahabari alimkamata mwandamanaji mmoja.

Kisa hicho kilikashifiwa na tume za kutetea haki za binadamu huku wakisema kuwa walikuwa wanaweka maisha ya wanahabari hatarini.

  • Tags

You can share this post!

Tanzania yailemea Kenya katika uvutaji bangi – Utafiti

Firat motoni kwa kupuuza wachezaji wa Gor, Tusker na Ingwe...

T L