• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 5:29 PM
Mahakama yarudishia Pasta Ezekiel nyota yake

Mahakama yarudishia Pasta Ezekiel nyota yake

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA kuu imemrejeshea nyota Pasta Ezekiel baada ya kusitisha utekelezaji wa agizo la serikali la kufutilia mbali leseni ya usajili wa kanisa lake la New Life lililoko Mavueni kaunti ya Kilifi.

Akimruhusu Pasta Odero kuendelea huduma ya kanisa lake, Jaji Jairus Ngaah alisema kanisa hilo lilifungwa kabla ya walalamishi kupewa muda wa kujitetea dhidi ya madai hawakuwa wakiwasilisha ripoti ya kila mwaka ya mwendelezo na huduma za kanisa hilo.

Jaji Ngaah alipiga breki hatua hiyo ya Serikali ya kuzima huduma za kanisa hilo linalotoa ajira kwa zaidi ya watu 8000 katika eneo la Mavueni na matawi mengine nchini.

“Baada ya kuwasikiza mawakili wa Pasta Ezekiel Odero pamoja na kuzingatia ushahidi uliowasilisha nimefikia uamuzi kesi hii iko na mashiko kisheria. Nasitisha utekelezaji wa gazeti rasmi la Serikali la Agosti 18, 2023 lililofutilia mbali leseni ya kuhudumu kwa kanisa la New Life lake Pasta odero,” Jaji Ngaah aliamuru.

Ngaah alielezwa na mawakili Martina Suiga , Shadrack Wambui na Danstan Omari kwamba “hatua ya serikali kufunga kanisa hilo ni njama za kupora mali na majengo ya kanisa hilo na hatimaye kuifunga.”

Katika ushahidi aliotoa mbele ya Jaji Ngaah,Bw Omari alimweleza Jaji Ngaa walalamishi Frankline Kilonzo, Bi Alice Nafula Wanyama na Pasta Odero hawakupewa fursa kueleza kilichojiri na kuwafanya wasiwasilishe ripoti za kila mwaka kwa msajili wa vyama vya ushirika kuhusu usimamizi wa kanisa hilo na uongozi wake.

PASTA Ezekiel Odero ambaye Kanisa lake limefutiliwa mbali amekata rufaa kupinga hatua hiyo akidai “hakupewa arifa ajitete kwa mujibu wa sheria.”

Rufaa hiyo iliwasilishwa na wakili Danstan Omari, akisema, Pasta Odero hakupewa muda kutetea kanisa lake huku akidai sheria hazikufuatwa.

Bw Omari aliwasilisha rufaa hiyo katika mahakama kuu na pia katika afisi ya Mkuu wa Sheria.
Bw Omari anayemwakilisha Pasta Odero na mawakili Cliff Ombeta, Sam Nyaberi na Martin Suiga waliele mahakama haki za Pasto, waumini Frankline Kilonzo na Nafula Wanyama walifgabishwa na hatua ya msajili wa mahakama kufunga kanisa hilo.

Mahakama ilifahamishwa msajili wa vyama vya ushirika alikaidi kifungu nambari 232 cha katiba kuhusu maadili na utekelezaji kazi kwa njia angavu.

Jaji Ngaah pia alielezwa Pasta Ngaah ameandika mabarua zadi ya 20 akiomba faili ya kanisa lake liwasilishwe ili aweke makaratasi ya kuripoti jinsi kanisa linaendelea.

Kufungwa kwa kanisaz hilo, Jaji Ngaah alielezwa kumeathiri wafanyakazi 8,000 walioajiriwa kujenga shule, uwanja wa ndege, chuo kikuu na shule ya kimataifa inayohudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 3,000.

Jaji Ngaah alimkosoa msajili wa vyama kwa kukandamiza haki za Pasta Ezekiel Odero na wafuasi wa kanisa lake zaidi ya 2 milioni.

Jaji huyo aliamuru kesi aliyoshtakiwa Past Odero na wafuasi wawili wa kanisa lake isikizwe Septemba 21, 2023.

Kufuatia agizo hilo kanisa hilo linaweza kuendelea na shughuli zake hadi pale kesi hiyo itasikizwa na kuamuliwa.

Mbali na kanisa la New Life serikali ilitia kufuli makanisa mengine manne.

Bw Omari alieleza Jaji Ngaah Kifungu nambari 12 za Sheria zinazothibiti mashirika ya kijamii kinasema “kabla kanisa au chama kufutiliwa mbali sharti maafisa wa chama hicho au shirika wajulishwe.”
Jaji huyo alielezwa wafuasu Zaidi

10milioni kutoka mataifa mbali mbali ya kigeni na humu nchini wanatarajiwa kuhudhuria “Meza ya Bwana (sakaramenti maalum) itakayoendelea kwa muda wa siku 14 kuanzia Agosti 20, 2023,” ndio wamiliki wake.

 

  • Tags

You can share this post!

Mzazi aishtaki shule kwa kuacha kunguni kuvamia wanafunzi

Wakazi wa vijiji vilivyoshambuliwa Lamu watafuta maeneo...

T L