• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 6:55 PM
Polisi aliyepora wafanyabiashara Sh2.8 milioni ashtakiwa

Polisi aliyepora wafanyabiashara Sh2.8 milioni ashtakiwa

Na JOSEPH NDUNDA

AFISA wa Polisi wa utawala ambaye aliwanyaka wafanyabiashara wawili kisha kuwaibia Sh2.8 milioni akidai yeye ni Kachero kutoka Idara ya Upelelezi Nchini (DCI) jana alishtakiwa kwa wizi wa mabavu kinyume cha sheria.

Geoffrey Kyalo Mwangangi anadaiwa aliwaibia Mohammed Sheikh na Shafe Omar pesa hizo katika makazi ya Lalucia Kileleshwa ambako aliwakamata karibu na makao makuu ya DCI mnamo Aprili 9.

Bw Mwangangi ambaye anafanya katika Kitengo cha CIPU kwenye jumba la Nyayo anadaiwa alitenda kosa hilo pamoja na wengine ambao hakuwa mahakamani, akiwemo askari ambaye anafanyikia kazi kwenye gereza la wanawake la Langata ambaye pia alinyakwa na maafisa wa DCI na hakuwa kortini.

Mshukiwa aliwakamata wawili hao Kileleshwa ambapo walikuwa wamealikwa kwa mazungumzo ya kibiashara na mwanaume ambaye pia baadaye ilibainika alikuwa mshirika wa afisa huyo wa polisi kwenye wizi huo.

Bw Mangangi anadaiwa alitishia kutumia vurugu dhidi ya walalamishi wakati wa wizi huo. Aliachiliwa kwa bondi ya Sh300,000 mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Makadara Lewis Gatheru baada ya kukanusha mashtaka dhidi yake

 

  • Tags

You can share this post!

Ichung’wah ashtakiwa na wakili Omari kwa matusi

Raila arejea nyumbani baada ya ziara ya Dubai

T L