• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
Raila na Karua kuzoa asilimia 60 ya kura za Mlima Kenya – Jubilee Kirinyaga

Raila na Karua kuzoa asilimia 60 ya kura za Mlima Kenya – Jubilee Kirinyaga

NA MWANGI MUIRURI

MWENYEKITI wa chama tawala cha Jubilee katika Kaunti ya Kirinyaga Bw Múríithi Kang’ara amesema kwamba mwaniaji wa urais kwa mrengo wa Azimio la Umoja Bw Raila Odinga atapata asilimia 60 ya kura za eneo la Mlima Kenya.

Aidha, Bw Kang’ara alisema kuwa ana fununu kwamba mgombeaji mwenza wa Bw Odinga atakuwa Bi Martha Karua ambaye akiwa na chama chake cha Narc-Kenya amejiunga na mrengo wa Azimio la Umoja.

Alisema kwamba hatua hiyo itawapa akina mama na wanawake wapigakura kwa ujumla, morali ya kupiga kura ya kujitambua.

“Bi Karua anatambulika na anaheshimika. Ataweza. Na tayari habari za yeye kuingia Azimio la Umoja zimepokelewa vyema. Ameongeza ubora mrengo wa Bw Odinga na kilele ni Kaunti ya Kirinyaga kuvuna unaibu wa urais,” akasema Bw Kang’ara.

Akiongea katika mji wa Kagio, Bw Kang’ara alisema kwamba ushirikiano wa Rais Uhuru Kenyatta, mabwanyenye na wanasiasa utahakikisha kuafikiwa kwa azma hiyo.

“Hawezi akaungwa mkono na mtandao huo halafu aambulie patupu. Bw Odinga ni nembo inayojulikana na iliyo na makali yake ya kipekee. Ni mwanasiasa ambaye amejishindia ufuasi wake na kile amekuwa akikosa ni ushawishi wa wadau muhimu Mlima Kenya ambao badala yake wamekuwa na mtandao unaofadhili njama za kumwangusha. Hayo ni ya kale sasa na safari hii tumemkumbatia,” akasema.

Bw Kang’ara alikuwa akiongea baada ya mkutano wa wawaniaji katika eneo hilo kwa chama cha Jubilee.

“Bw Odinga ako na serikali nyuma yake. Yeye ni kama Rais tu. Ukimwongeza mabwanyenye wetu na wanasiasa hawa wote walio nyuma yake, ile asilimia tatu ya kura ambayo amekuwa akipata Mlima Kenya itapanda kwa kasi na hivyo ninawasihi watu wetu wazoee mapema kumtambua kama Rais wa Tano wa Taifa hili la Kenya,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Vijana sasa walia usajili wa polisi haukuwa wa haki

Joto kali Azimio, Kenya Kwanza wakimenyana Magharibi

T L