• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:24 PM
Serikali kutathmini VAT inayotozwa mbegu za mboga

Serikali kutathmini VAT inayotozwa mbegu za mboga

Na SAMMY WAWERU

SERIKALI itatathmini pendekezo la kupunguza au hata kuondoa ushuru (VAT) unaotozwa mbegu za mboga.

Wakulima, kampuni na mashirika yanayoendeleza kilimo na na kupiga jeki sekta hii, wamekuwa wakilalamikia ushuru wa juu unaotozwa mbegu za mboga.

Ada hizo kulingana na wakulima, zimeendelea kulemaza jujudi za uzalishaji wa mboga nchini, mataifa jirani yakitajwa kuwa kifua mbele katika ukuzaji.

Kwa mujibu wa malalamishi yao, gharama ya juu kununua mbegu za mboga inawanyima fursa kushiriki masoko ya kimataifa na ambayo yana ushindani mkuu kimapato.

Akikiri changamoto zinazokumba ukuzaji wa mboga Kenya, Dkt Oscar Magenya, ambaye ni Karani Mtafiti wa Masuala ya Kilimo katika Wizara ya Kilimo, amesema serikali imeweka mipango na mikakati kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora na zilizoidhinishwa.

“Kwa sasa, tunashughulikia kupunguza au hata kuondoa VAT inayotozwa mbegu za mboga,” akasema Dkt Magenya, akizungumza jijini Nairobi katika hafla iliyoandaliwa na wadauhusika sekta ya kilimo.

Kulingana na afisa huyo, hatua ya kupunguza ushuru wa mbegu za mboga utasaidia kushusha gharama ya ukuzaji.

“Isitoshe, itatusaidia kushiriki masoko ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla,” akaelezea.

Bei ya pembejeo Kenya; mbegu, fatalaiza na dawa kukabiliana na kero ya wadudu na magonjwa inaendelea kuwa ghali, mfumko ambao unakwamisha jitihada za wakulima.

Fatalaiza kwa mfano, bei yake imepanda mara dufu ikilinganishwa na ilivyokuwa ikiuzwa miaka miwili iliyopita.

DAP mfuko wa kilo 50 unauzwa Sh5,200, CAN Sh4,200 na Urea Sh6,200 kipimo ambacho awali kilikuwa chini ya Sh3, 000.

“Hii ndiyo bei ghali zaidi katika tajiriba yangu ya miaka 30 kwenye kilimo. Wengine wakisherehekea Jamhuri, mimi niko shambani nikikadiria hasara,” akasema mbunge wa Mathira, Bw Rigathi Gachagua wakati wa maadhimisho ya Jamhuri Dei 2021.

Huku mbunge huyo akihoji amepanga kuendeleza shughuli za kilimo kama mradi wa kujiendeleza kimaisha baada ya kustaafu, alisema ni hasara kwa wakulima wanaofanya kilimo-biashara kutokana na bei ghali ya pembejeo, bei ya mazao ikisalia ilipokuwa kitambo, miaka nenda miaka rudi.

Kando na kutozwa ushuru, mbegu zimekumbwa na kero ya utengenezaji wa zile bandia.

You can share this post!

Refa anayeibukia na mwenye maono ya kupiga shughuli...

Man-United waripoti visa vingi zaidi vya corona

T L