• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Waiguru hatarini kupoteza nyumba

Waiguru hatarini kupoteza nyumba

NA RICHARD MUNGUTI

GAVANA wa Kirinyaga Bi Anne Waiguru anakabiliwa na tisho ya kupoteza nyumba yake ya kifahari ya thamani ya Sh200 milioni aliyonunua 2015.

Hii ni baada ya kuibuka kuwa mkataba wa ununuzi wa makazi hayo ya Bi Waiguru ulikuwa kinyume cha maagizo ya korti ya 2013.

Katika ushahidi uliowasilishwa Ijumaa katika Mahakama Kuu na wakili Chris Kabiro, Bi Waiguru alinunua jumba hilo 2015 kinyume cha maagizo ya Jaji Eric Ogolla la Desemba 2013 kwamba isiuzwe.

Bw Kabiro anayeomba Mahakama Kuu itupilie mbali kesi Bi Waiguru aliyowasilisha akiomba Kampuni ya Kihingo Village (Waridi Gardens) Limited ilazimishwe kukamilisha mkataba wa mauzo ndipo ailipe Sh40milioni zilisosalia ili aimiliki kabisa na kupewa hati ya umiliki.

Bi Waiguru ameeleza mahakama kwamba alikubaliana na Kihingo kupitia kwa Mbunge wa zamani wa Tetu Ndung’u Gethenji, ainunue jumba hilo kwa bei Sh80,687,170.

Amefichua alimpa Gethenji zaidi ya Sh40 milioni.

Lakini mkurugenzi mwingine wa Kihingo Bw Gitahi Gethenji (nduguye Ndung’u) amesema Bi Waiguru alinunua nyumba hiyo kimakosa kwa vile kulikuwa na agizo la Jaji Ogolla isiuzwe.

Gitahi amesema Waiguru alikubaliana na Ndung’u kununua nyumba hiyo wakati ambapo Mahakama Kuu ilikuwa imezima uuzaji.

Kesi ya jumba hilo itasikilizwa Novemba 22, 2022.

You can share this post!

Mwili wa mlinzi wapatikana ndani ya darasa

KOMBE LA DUNIA 2022: Jacob ‘Ghost’ Mulee...

T L