• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 8:11 PM
Wakazi wa Gatundu wapokea miche ya macadamia

Wakazi wa Gatundu wapokea miche ya macadamia

NA LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa Gatundu Kusini wapatao 5,000 walipokea miche ya macadamia ili kuboresha kilimo cha zao hilo.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘ Wajungle’ Wainaina, aliongoza zoezi hilo huku akiwahimiza wakazi hao kukumbatia kilimo hicho cha macadamia akikitaja kama dhahabu ya mkulima.

“Ninawahimiza mfanye hima kuzingatia upanzi wa miche ya macadamia kwa sababu baada ya miaka miwili hivi mtavuna zao la kuingiza pesa kwa wingi. Hata nitakuwa tayari kuwatafutia soko kwa nchi za ng’ambo,” alijitetea mbunge huyo.

Bw ‘Wajungle’ ambaye anawania kuwa gavana wa Kiambu aliwarai wakazi hao kumchagua ili aweze kuboresha maisha ya wakazi wote wa Gatundu Kusini na Kaskazini.

“Mimi kama mzaliwa wa eneo hili ninaelewa shida zenu. Eneo la Thika tayari linajulikana vyema nchini kote kutokana na utumizi bora wa fedha za maendeleo ya NG-CDF,” alifafanua Bw ‘Wajungle’ na kuongeza “ni lazima muwe na mwelekeo na muwachague viongozi wanaoelewa shida za wananchi kwa ujumla.”

Alisema kaunti ya Kiambu hupokea Sh10 bilioni za maendeleo kila mwaka, ambazo inaweza kugeuza maisha ya wakazi wote wa Kiambu.

Alisema iwapo atapata nafasi ya kuwa gavana ataweka BIMA ya afya kuwa Sh 20 kwa kila mkazi na mpango huo utaboresha hali ya afya ya kila mmoja.

Alisema atafanya juhudi kuona ya kwamba barabara kama miundo msingi inajengwa zaidi ya kilomita 500 ili kupanua hali ya usafiri na kuboresha biashara zote katika kaunti yote ya Kiambu.

Bw ‘Wajungle’ aliwataka wakazi hao kufanya uamuzi wa busara wanapopiga kura Agosti 9, 2022.

Alitoa wito kwa Wakenya wote popote walipo kuwachagua viongozi wenye rekodi njema na maadili mema.

“Ili tuweze kuendesha nchi isiyo na rushwa, ni sharti tuwateme viongozi wote wafisadi, na kuwachagua wenye nia njema na maadili mema,” alieleza Bw Wajungle.

Baadhi ya maeneo aliyozuru alipopeana miche ni Gachege, Githunguri na Gatundu Kusini.

Mbunge huyo alimteua mgombea mwenza wake ambaye ni Bi Anne Nyokabi Gatheca na anatumia tikiti ya kujitegemean(Independent).

Bi Gatheca aliwashauri wakulima wasikubali kuingiliwa na mawakala ambao hutaka kuwanyanyasa wanapopata mazao yao.

  • Tags

You can share this post!

Ruto awaahidi kinamama vinono akiunda serikali

Jaji Mkuu Koome ataka Uhuru atimuliwe kwa kutoteua majaji...

T L