• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Wakenya tulieni tuko na ‘plan’, asema Alfred Mutua

Wakenya tulieni tuko na ‘plan’, asema Alfred Mutua

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema kwamba swala la kupanda kwa gharama ya maisha si tatizo la Kenya peke yake kwani hata mataifa mengine duniani yanakabiliwa na changamoto hiyo.

Waziri wa Masuala ya Kigeni Dkt Alfred Mutua, akihutubu jijini Nairobi, amesema katika baadhi ya ziara za kigeni akiandamana na Rais William Ruto barani Ulaya, kulikuwa na maandamano katika baadhi ya mataifa kwa sababu ya kupanda kwa gharama ya maisha.

“Ni kweli kwamba kuna tatizo la uhaba wa chakula kote duniani na suala hili la uhaba wa chakula ni ajenda inayozungumziwa kote nchini. Lakini tuko pazuri kwa sababu tuna mpango kabambe wa kukabiliana na changamoto hii,” amesema Dkt Mutua.

Ameahidi kwamba ingawa hali inaonekana kuwa ngumu wakati huu, mambo yanabadilika na hivi karibuni yatakuwa sawa.

Waziri Mutua amesikitika akisema maandamano yaliyoitishwa na muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga hayatasaidia kuimarisha hali. Badala yake, amesema maandamano yanasababisha akina mama wanaojituma kazini na wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara kuogopa kufika katika sehemu zao za kawaida za kutafuta riziki kwa sababu kuna wahuni wanaojitokeza kupora mali.

Amedai kwamba Azimio wanaitisha maandamano wakitaka nusu-mkate serikalini.

Aidha anasema Kenya iko salama na madai kwamba watu 23 walipoteza maisha yao kwenye maandamano wiki jana ni propaganda.

“Inasikitisha kwamba mnamo Julai 14, 2023, msemaji wa Shirika la Haki la Umoja wa Mataifa alitoa taarifa kuashiria kuna machafuko makubwa nchini na kwamba maafisa walitumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamanaji. Hii inapotosha na si sahihi,” amesema.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge wa UDA afurushwa Kisii akijaribu kusitisha...

Cleophas Malala aongoza UDA ‘kulinda’ mali ya...

T L