• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:50 AM
Wanafunzi wanane katika kituo cha kurekebisha tabia wapata ufadhili waendelee na elimu ya upili

Wanafunzi wanane katika kituo cha kurekebisha tabia wapata ufadhili waendelee na elimu ya upili

Na SAMMY KIMATU

WANAFUNZI wanane katika kituo kimoja cha kurekebisha tabia katika Kaunti ya Nairobi waliofanya vizuri katika mtihani wa KCPE 2020 wamepata ufadhili wa masomo katika shule za upili.

Ufadhili huo umetolewa na Kituo cha Mukuru Promotion Centre (MPC) kinachosimamiwa na Sisters of Mercy-Kenya Province.

Akiongea na Taifa Leo mnamo Jumanne, Mkurungezi Mkuu wa MPC, Mtawa Mary Killeen alisema watoto hao ni wa Kituo cha Mary Immaculate (MIRC) kilichoko South B, kaunti ndogo ya Starehe.

Aidha, mtawa Killeen aliongeza kwamba wanafunzi waliobahatika na ufadhili huo ni mseto wa waliosemea katika shule za msingi za St Catherine, St Paul na St Peter.

Vile vile, Mtawa Killeen alikariri kwamba MPC itagharimia karo ya wanane hao kusoma kutoka Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne.

“Kituo cha MPC hulenga kuinua elimu ya watoto werevu wasiobahatika kwa jamii kupitia kuwasomesha kwa kugharamia karo yao katik shule ya upili,” Mtawa Killeen alisema.

Kando na hayo, wanafunzi saba miongoni mwa wote wanane walipata kati ya alama 257 na alama 372 huku mmoja akipata alama 223.

Kutokana na mazingira ya wanakotoka watoto hao, kituo cha MPC kilisimamia pia malezi na urekebishaji tabia wakikakaa katika kituo cha MIRC.

“Huku wakisomea katika shule za msingi tajika, watoto hawa walikuwa wakiishi katika kituo chetu cha MIRC na kupata ushauri nasaha pia,” Mtawa Killeen akaongeza.

Kadhalika, mtawa Killeen alisema MPC ina nafasi zaidi kwa wanafunzi wengine wakati watahiniwa wa KCPE kutoka shule nne katika maeneo ya Mukuru, zinazofadhiliwa na kituo cha MPC, wanaposubiri kupokea barua za kujiunga na shule za upili.

  • Tags

You can share this post!

Fahamu nani atamenyana na nani kwenye robo-fainali za Euro

Mwanataekwondo Ogallo ashinda uandishi wa insha ya Olimpiki...